Luqman Maloto: Sauti kutoka kaburini kwa Ali Kibao ifike hadi ikulu kwa Rais Samia

magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
11,075
Reaction score
24,634
KATA ya Mzingani, Tanga, nyumbani kwa Ali Mohammed Kibao, ni eneo la tukio. Watu wanazomea, makofi yanapigwa na mayowe ya kushangilia. Ajabu, mkusanyiko ni wa msiba. Shughuli ni mazishi.

Ali ndiye kichwa cha habari cha msiba. Amefariki dunia. Mazingira ya kifo yanaogofya kupita kiasi. Ali ameuawa. Mauaji yake ni ya kikatili kupindukia. Ripoti ya uchunguzi inaonesha alipigwa na kuumizwa kichwani. Hadi fuvu limeumia. Kisha, akamwagiwa tindikali usoni.

Kisa nini watu wazomee msibani? Nini sababu ya makofi kwenye shughuli ya mazishi? Maswali yote mawili jibu lake ni moja; hisia! Kifo cha Ali kinaumiza, kinashangaza, kinatatanisha. Mazingira yake ndiyo kiini cha utata.

Binadamu yeyote hapaswi kutendewa unyama aliofanyiwa Ali. Mtu unapanda basi, usafiri wa umma. Watu wenye bunduki wanavamia gari. Wanajitambulisha kuwa maofisa wa usalama. Wanamfunga pingu. Wanamshusha. Wanakwenda kumpiga hadi kumuua. Kama haitoshi, wanam-mwagia tindikali. Ndivyo Ali alivyouawa.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, amefika msibani kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan. Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, anamwambia Masauni: “Usiende tena kwenye msiba wa mtu aliyetekwa.” Watu wanapiga makofi.

Lema akaendelea kwa kumwambia Masauni kuwa alipaswa kuwa ameshajiuzulu. Hapo yakafuata makofi pamoja na mayowe. Ali ni Mwislam. Mazishi yanaongozwa kwa mila na desturi za dini ya Kiislam. Shehe, anayeongoza ibada ya mazishi, anausia kutopiga makofi msibani.

Inafuata zamu ya Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika. Pamoja na kusimulia mema ya Ali, naye anamtaka Masauni kuwajibika. Kwa mara nyingine, umati unalipuka kwa makofi na vifijo. Mnyika pia anataka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene, naye ajiuzulu. Makofi mengine yakapigwa, watu wakashangilia.

Maelekezo ya kutopiga makofi na kushangilia, hayakuzingatiwa. Ukawadia wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Batilda Buriani. Alipata wakati mgumu kuzungumza, maana alikutana na zomeazomea. Batilda ni mkomavu kisiasa, vinginevyo wazomeaji wangeweza kumtoa kwenye mstari. Aliweza kubaki mstarini hadi alipomaliza hotuba yake.

Soma Pia:
Waziri Masauni alikuwa kwenye wakati mgumu zaidi. Kuna wakati alilazimika kukatisha hotuba yake, sababu wazomeaji walimzidi nguvu. Baada ya zogo kuwa kubwa, ilibidi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, asimame kutuliza fujo zilizokuwepo. Akawataka watu kutulia na kumsikiliza Masauni. Angalau baada ya hapo, Masauni aliweza kuhutubia hadi mwisho.

Mbowe alipozungumza, makofi na sauti za ushangiliaji vilirejea. Jibu la kwa nini viongozi wa Serikali walizomewa na wa Chadema walishangiliwa, wala halina mzunguko. Dhahiri, imani ya watu kwa Serikali kuhusiana na Ali kutekwa na kuuawa, ni ndogo mno. Pengine, hawaiamini kabisa.

Taswira ya mazishi ya Ali, ungedhani ni Wapalestina, jinsi ambavyo huzika ndugu zao wanaouawa na Wayahudi. Wapalestina hubeba miili ya ndugu, vijana na watoto wao ambao huuawa, kwa hisia na sauti kubwa kumwelekea Mungu ili kufikisha ujumbe kwa ulimwengu kwamba wanatendewa ukatili na wanauawa kinyama, hivyo hawana wa kumlilia zaidi ya aliye juu.

Ndivyo ilivyokuwa katika mazishi ya Ali. Alikuwa mwanachama wa Chadema. Mwanamikakati na kiungo muhimu kwenye sekretarieti ya Chadema. Nadharia kuu ya kutekwa na kuuawa kwa Ali ni uanachama na uhusika wake kimkakati ndani ya Chadema. Hiyo ndiyo sababu viongozi wa Chadema wanarusha lawama moja kwa moja kwa dola, juu ya kifo cha Ali.

Majuma yamekatika tangu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chadema (Bavicha), Wilaya ya Temeke, Deusdedith Soka na wenzake wawili, Jacob Mlay na Frank Mbise, wanyakuliwe, wapelekwe kusikojulikana. Kiongozi wa Chadema, wilaya ya Sumbawanga, Rukwa, Dioniz Kipanya, naye inadaiwa alitekwa, hajulikani alipo.

Siku Ali anatekwa, ilikuwa inatimia miaka saba tangu Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, Tundu Lissu, aliposhambuliwa kwa risasi, ambazo zimemsababisha ulemavu wa maisha hadi leo. Tukio la Lissu limebaki kuwa moja ya matukio yaliyokosa majibu. Waliomshambulia hawajatambuliwa, hawajafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mwandishi wa habari Azory Gwanda, anakaribia kutimiza miaka saba tangu alipotekwa. Kada wa Chadema, Ben Saanane, Novemba 2024, atafunga mwaka wa nane, tokea alipochukuliwa. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kanguye, Julai 2024, alikamilisha miaka saba, tangu aliponyakuliwa.

Afrika, eneo ambalo ni hatari kabisa kwa usalama wa raia ni Ghuba ya Guinea, ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa vifo, utekaji watu na hata ubakaji wa wanawake Afrika Magharibi. Kutoka Ghuba ya Guinea, hadi mataifa mengi ya Afrika yenye usalama mdogo wa raia, vyanzo vyake huwa viwili tu; mosi, vita vya kiraia, pili, kufeli kwa Serikali.

Nigeria, Liberia, Guinea Bissau, Libya, Sierra Leon, Ivory Coast, Jamhuri ya Kongo (Brazzaville), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ni mifano ya mataifa yenye usalama mdogo wa raia, kwa mujibu wa ripoti za dunia. Sababu kubwa ni historia ya nchi hizo kupigana vita vya kiraia, kisha kushindwa kwa Serikali kutuliza hali ya nchi.

Tanzania haina historia ya kupigana vita ya kiraia, halafu kwa jicho la juu, nchi imekuwa ikipita salama nyakati za uchaguzi na mabadilishano ya madaraka. Swali ambalo pengine linashangaza wengi ni kwa nini utekaji na mauji vinashika kasi Tanzania? Hapa hatujaingiza kwenye mjadala matukio ya mauaji ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji (Mkiru).

Alisema Mbowe msibani kwa Ali, kuwa inawezekana waliokuwa wanazomea wakatafsiriwa kuwa hawakuwa na nidhamu kwa viongozi wa Serikali, lakini akawataka kufanya marejeo ya matukio mfululizo ya watu kutekwa, ambayo hayajapatiwa majibu. Kauli hii ni ya kweli kabisa.

Tukio la kijana mwanaharakati, Edgar Mwakabela “Sativa”, kutekwa na kutupwa msituni Katavi, bado halina majibu. Mkusanyiko wa matukio yote hadi aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Madaktari, Dk Steven Ulimboka, aliyepigwa, akavunjwa mbavu, akang’olewa meno na kucha Juni 2012, yanatengeneza hali ya kutoamini dola.

Shughuli za mazishi zilifanyika Mzingani, Tanga. Kisha Ali alisafirishwa kilometa 13.2 hadi kijijini kwake Darigube, Tanga, alikozikwa. Sauti zilizosikika mazikoni Darigube na mazishini Mzingani, hisia na maumivu yake, zifike hadi Ikulu, kwa Rais Samia. Watu wanapoteza imani na vyombo vyao vya usalama, sababu matukio ya nyuma hayana majibu.

Mwisho kabisa, Rais Samia anapaswa kutambua kuwa yeye ndiye mlinzi mkuu wa usalama wa raia. Hivyo, matukio yote ya utekaji na mauaji, jinsi majibu yasivyopatikana, anayetazamwa ni yeye, Amiri Jeshi Mkuu.

Tanzania iliyoimbwa na kunakshiwa kwa jina la “kisiwa cha amani”, imekuwa dola hatafi kwa usalama kwa raia wake. Yote yatasahaulika, kumbukumbu zitabaki ni wakati gani Watanzania walitekwa na kuuawa hovyo. Kipindi gani ukatili huu wa kumwagiana tindikali ulitokea. Vifo vitokee, mateka waongezeke, yapo majina yatatajwa vizazi kwa vizazi.

Mungu hakuumba waja wake, akawaleta duniani, waje wateswe na kuuawa na binadamu wenzao. Mungu hakumaanisha Tanzania liwe taifa la dhuluma ya uhai. Namwamini mno Mungu wa Tanzania. Hakunyamaza nyuma, hatanyamaza sasa. Ni Mungu wa ulimwengu, hajawahi kutoa kibali kwa wauaji, watekaji na watesaji.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Umeupiga mwingi mkuu Luqman Maloto.
 
Viongozi wa kisiasa siku hizi muone aibu mnapokuwa majukwaani na kusema Tanzania ni nchi ya amani sio kweli nyie mmeinajisi bendera ya taifa na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
The assassination of this person was extremely brutal and diabolical.
Very sad indeed!

Mauaji ya kikatili aliyofanyiwa mtu huyu ni zaidi ya ushetani.
Na ukifuatilia kwa undani zaidi hapo baadaye siku chache zijazo unaweza kuja kugundua kwamba watu wao walioshiriki au kuhusika katika 'mission' ya kutenda ushetani huo wanapewa promotion ya kupandishwa vyeo kwenye Ofisi zao eti kwa sababu 'wametekeleza majukumu yao waliyopewa vizuri Sana.'
 
Wanajulikana
 
'mission' ya kutenda ushetani huo wanapewa promotion ya kupandishwa vyeo kwenye Ofisi zao eti kwa sababu 'wametekeleza majukumu yao waliyopewa vizuri Sana.'
Kinyume chake kina uzito zaidi.
Hatma ya watu wa namna hiyo huwa ni kuondolewa moja kwa moja, kwa sababu wakibaki hai kuna siku wataropoka.
 
KATA ya Mzingani, Tanga, nyumbani kwa Ali Mohammed Kibao, ni eneo la tukio. Watu wanazomea, makofi yanapigwa na mayowe ya kushangilia. Ajabu, mkusanyiko ni wa msiba. Shughuli ni mazishi.

Ali ndiye kichwa cha habari cha msiba. Amefariki dunia. Mazingira ya kifo yanaogofya kupita kiasi. Ali ameuawa. Mauaji yake ni ya kikatili kupindukia. Ripoti ya uchunguzi inaonesha alipigwa na kuumizwa kichwani. Hadi fuvu limeumia. Kisha, akamwagiwa tindikali usoni.

Kisa nini watu wazomee msibani? Nini sababu ya makofi kwenye shughuli ya mazishi? Maswali yote mawili jibu lake ni moja; hisia! Kifo cha Ali kinaumiza, kinashangaza, kinatatanisha. Mazingira yake ndiyo kiini cha utata.

Binadamu yeyote hapaswi kutendewa unyama aliofanyiwa Ali. Mtu unapanda basi, usafiri wa umma. Watu wenye bunduki wanavamia gari. Wanajitambulisha kuwa maofisa wa usalama. Wanamfunga pingu. Wanamshusha. Wanakwenda kumpiga hadi kumuua. Kama haitoshi, wanam-mwagia tindikali. Ndivyo Ali alivyouawa.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, amefika msibani kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan. Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, anamwambia Masauni: “Usiende tena kwenye msiba wa mtu aliyetekwa.” Watu wanapiga makofi.

Lema akaendelea kwa kumwambia Masauni kuwa alipaswa kuwa ameshajiuzulu. Hapo yakafuata makofi pamoja na mayowe. Ali ni Mwislam. Mazishi yanaongozwa kwa mila na desturi za dini ya Kiislam. Shehe, anayeongoza ibada ya mazishi, anausia kutopiga makofi msibani.

Inafuata zamu ya Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika. Pamoja na kusimulia mema ya Ali, naye anamtaka Masauni kuwajibika. Kwa mara nyingine, umati unalipuka kwa makofi na vifijo. Mnyika pia anataka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene, naye ajiuzulu. Makofi mengine yakapigwa, watu wakashangilia.

Maelekezo ya kutopiga makofi na kushangilia, hayakuzingatiwa. Ukawadia wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Batilda Buriani. Alipata wakati mgumu kuzungumza, maana alikutana na zomeazomea. Batilda ni mkomavu kisiasa, vinginevyo wazomeaji wangeweza kumtoa kwenye mstari. Aliweza kubaki mstarini hadi alipomaliza hotuba yake.

Soma Pia:
Waziri Masauni alikuwa kwenye wakati mgumu zaidi. Kuna wakati alilazimika kukatisha hotuba yake, sababu wazomeaji walimzidi nguvu. Baada ya zogo kuwa kubwa, ilibidi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, asimame kutuliza fujo zilizokuwepo. Akawataka watu kutulia na kumsikiliza Masauni. Angalau baada ya hapo, Masauni aliweza kuhutubia hadi mwisho.

Mbowe alipozungumza, makofi na sauti za ushangiliaji vilirejea. Jibu la kwa nini viongozi wa Serikali walizomewa na wa Chadema walishangiliwa, wala halina mzunguko. Dhahiri, imani ya watu kwa Serikali kuhusiana na Ali kutekwa na kuuawa, ni ndogo mno. Pengine, hawaiamini kabisa.

Taswira ya mazishi ya Ali, ungedhani ni Wapalestina, jinsi ambavyo huzika ndugu zao wanaouawa na Wayahudi. Wapalestina hubeba miili ya ndugu, vijana na watoto wao ambao huuawa, kwa hisia na sauti kubwa kumwelekea Mungu ili kufikisha ujumbe kwa ulimwengu kwamba wanatendewa ukatili na wanauawa kinyama, hivyo hawana wa kumlilia zaidi ya aliye juu.

Ndivyo ilivyokuwa katika mazishi ya Ali. Alikuwa mwanachama wa Chadema. Mwanamikakati na kiungo muhimu kwenye sekretarieti ya Chadema. Nadharia kuu ya kutekwa na kuuawa kwa Ali ni uanachama na uhusika wake kimkakati ndani ya Chadema. Hiyo ndiyo sababu viongozi wa Chadema wanarusha lawama moja kwa moja kwa dola, juu ya kifo cha Ali.

Majuma yamekatika tangu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chadema (Bavicha), Wilaya ya Temeke, Deusdedith Soka na wenzake wawili, Jacob Mlay na Frank Mbise, wanyakuliwe, wapelekwe kusikojulikana. Kiongozi wa Chadema, wilaya ya Sumbawanga, Rukwa, Dioniz Kipanya, naye inadaiwa alitekwa, hajulikani alipo.

Siku Ali anatekwa, ilikuwa inatimia miaka saba tangu Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, Tundu Lissu, aliposhambuliwa kwa risasi, ambazo zimemsababisha ulemavu wa maisha hadi leo. Tukio la Lissu limebaki kuwa moja ya matukio yaliyokosa majibu. Waliomshambulia hawajatambuliwa, hawajafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mwandishi wa habari Azory Gwanda, anakaribia kutimiza miaka saba tangu alipotekwa. Kada wa Chadema, Ben Saanane, Novemba 2024, atafunga mwaka wa nane, tokea alipochukuliwa. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kanguye, Julai 2024, alikamilisha miaka saba, tangu aliponyakuliwa.

Afrika, eneo ambalo ni hatari kabisa kwa usalama wa raia ni Ghuba ya Guinea, ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa vifo, utekaji watu na hata ubakaji wa wanawake Afrika Magharibi. Kutoka Ghuba ya Guinea, hadi mataifa mengi ya Afrika yenye usalama mdogo wa raia, vyanzo vyake huwa viwili tu; mosi, vita vya kiraia, pili, kufeli kwa Serikali.

Nigeria, Liberia, Guinea Bissau, Libya, Sierra Leon, Ivory Coast, Jamhuri ya Kongo (Brazzaville), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ni mifano ya mataifa yenye usalama mdogo wa raia, kwa mujibu wa ripoti za dunia. Sababu kubwa ni historia ya nchi hizo kupigana vita vya kiraia, kisha kushindwa kwa Serikali kutuliza hali ya nchi.

Tanzania haina historia ya kupigana vita ya kiraia, halafu kwa jicho la juu, nchi imekuwa ikipita salama nyakati za uchaguzi na mabadilishano ya madaraka. Swali ambalo pengine linashangaza wengi ni kwa nini utekaji na mauji vinashika kasi Tanzania? Hapa hatujaingiza kwenye mjadala matukio ya mauaji ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji (Mkiru).

Alisema Mbowe msibani kwa Ali, kuwa inawezekana waliokuwa wanazomea wakatafsiriwa kuwa hawakuwa na nidhamu kwa viongozi wa Serikali, lakini akawataka kufanya marejeo ya matukio mfululizo ya watu kutekwa, ambayo hayajapatiwa majibu. Kauli hii ni ya kweli kabisa.

Tukio la kijana mwanaharakati, Edgar Mwakabela “Sativa”, kutekwa na kutupwa msituni Katavi, bado halina majibu. Mkusanyiko wa matukio yote hadi aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Madaktari, Dk Steven Ulimboka, aliyepigwa, akavunjwa mbavu, akang’olewa meno na kucha Juni 2012, yanatengeneza hali ya kutoamini dola.

Shughuli za mazishi zilifanyika Mzingani, Tanga. Kisha Ali alisafirishwa kilometa 13.2 hadi kijijini kwake Darigube, Tanga, alikozikwa. Sauti zilizosikika mazikoni Darigube na mazishini Mzingani, hisia na maumivu yake, zifike hadi Ikulu, kwa Rais Samia. Watu wanapoteza imani na vyombo vyao vya usalama, sababu matukio ya nyuma hayana majibu.

Mwisho kabisa, Rais Samia anapaswa kutambua kuwa yeye ndiye mlinzi mkuu wa usalama wa raia. Hivyo, matukio yote ya utekaji na mauaji, jinsi majibu yasivyopatikana, anayetazamwa ni yeye, Amiri Jeshi Mkuu.

Tanzania iliyoimbwa na kunakshiwa kwa jina la “kisiwa cha amani”, imekuwa dola hatafi kwa usalama kwa raia wake. Yote yatasahaulika, kumbukumbu zitabaki ni wakati gani Watanzania walitekwa na kuuawa hovyo. Kipindi gani ukatili huu wa kumwagiana tindikali ulitokea. Vifo vitokee, mateka waongezeke, yapo majina yatatajwa vizazi kwa vizazi.

Mungu hakuumba waja wake, akawaleta duniani, waje wateswe na kuuawa na binadamu wenzao. Mungu hakumaanisha Tanzania liwe taifa la dhuluma ya uhai. Namwamini mno Mungu wa Tanzania. Hakunyamaza nyuma, hatanyamaza sasa. Ni Mungu wa ulimwengu, hajawahi kutoa kibali kwa wauaji, watekaji na watesaji.

Ndimi Luqman MALOTO
Umeeleza vizuri sana hata sisi ambao hatukufika msibani tumejuwa msiba ulivyo kwenda. Hapa cha kujifuza kikubwa ni kutambuwa kuwa kiongozi sio kukaria office za uuma na kutembelea magari makubwa yaliyo nunuliwa kwa kodi za wananchi. Wala sio kupewa majina ya vyeo kama waziri au raisi. Uongozi na heshima vinajegwa kwa kwa matendo mema na unyenyekevu mkubwa kwa unao waongoza. Ndio maana vigozi wa serikali wamezomewa kama vibaka msibani. Na watu kama Mbowe wasio kuwa na cheo chochote serikalini walipewa heshima ya kusikilizwa kwa makini.
 
Ulevi wa madaraka na ulimbukeni ni moja ya sababu za kutokea kwa haya matukio.
 
Back
Top Bottom