LGE2024 Lushoto waongeza vituo vya kupigia kura

LGE2024 Lushoto waongeza vituo vya kupigia kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Halmashauri ya Lushoto imebidi kuongeza vituo vya kupigia kura 64 katika maeneo mbalimbali kutokana na kuwepo malalamiko ya baadhi ya wananchi kuwa kuna sehemu vituo vipo mbali na hawataweza kufika huko.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Lushoto Ikupa Mwasyoge, leo Jumanne Novemba 26,2024 ameeleza kuwa vituo vya kupiga kura vimeongezeka kutoka 941 hadi 1,005.

Ameeleza kuwa baada ya kupokea malalamiko hayo ofisi yake iliyafikisha kwenye mamlaka husika, ambao baada ya kuona umuhimu wake walikubaliwa kuongeza, vituo na kufanya vituo kufikia idadi ya 1,005.

Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Msimamizi huyo anasema maandalizi yote kwa ajili ya uchaguzi huo yamekamilika hukuakiwahimiza wananchi hasa vijana, kujitokeza kwa wingi kupiga kura, kwani ni haki yao ya msingi.

Kuhusu vyama vya siasa, amebainisha kuwa vyama vinne CCM, Chadema, CUF, na ACT, ndio vinashiriki uchaguzi kwenye eneo hilo na tayari vimeleta mawakala wao ambao wameapishwa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo.

Novemba 27,mwaka huu Watanzania watafanya uchaguzi kwaajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na wajumbe wake, nafasi ambayo itadumu kwa miaka mitano hadi uchaguzi mwingine.
 
Kumbe mawakala wa vyama vyote wapo, haya Hatuhitaji kelele za tumeibiwa kura
 
Basi lushoto kuna watu mpaka vyumbani kwao wanakolala wamebandika mapicha ya ccm tena ya tangu kikwete, Magufuli nk. Wao wanachojua kule ni ccm tu basi vyama vingine vitaleta vurugu
Sasa katika jamii kama hiyo utashindwaje kupata mawakala hata wa kutengeneza?
 
Back
Top Bottom