Halmashauri ya Lushoto imebidi kuongeza vituo vya kupigia kura 64 katika maeneo mbalimbali kutokana na kuwepo malalamiko ya baadhi ya wananchi kuwa kuna sehemu vituo vipo mbali na hawataweza kufika huko.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Lushoto Ikupa Mwasyoge, leo Jumanne Novemba 26,2024 ameeleza kuwa vituo vya kupiga kura vimeongezeka kutoka 941 hadi 1,005.
Msimamizi huyo anasema maandalizi yote kwa ajili ya uchaguzi huo yamekamilika hukuakiwahimiza wananchi hasa vijana, kujitokeza kwa wingi kupiga kura, kwani ni haki yao ya msingi.
Kuhusu vyama vya siasa, amebainisha kuwa vyama vinne CCM, Chadema, CUF, na ACT, ndio vinashiriki uchaguzi kwenye eneo hilo na tayari vimeleta mawakala wao ambao wameapishwa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo.
Novemba 27,mwaka huu Watanzania watafanya uchaguzi kwaajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na wajumbe wake, nafasi ambayo itadumu kwa miaka mitano hadi uchaguzi mwingine.
Basi lushoto kuna watu mpaka vyumbani kwao wanakolala wamebandika mapicha ya ccm tena ya tangu kikwete, Magufuli nk. Wao wanachojua kule ni ccm tu basi vyama vingine vitaleta vurugu
Sasa katika jamii kama hiyo utashindwaje kupata mawakala hata wa kutengeneza?