Uchaguzi 2020 Lusinde: Mimi nilikuwa na Lissu Bungeni, hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndiyo maana nilikuwa namuita Malalamiko FC

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lusinde alimnyoshea kidole mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu akimweleza kuwa anapaswa kuzungumzia sera na kuwaelezea atawafanyia nini wananchi badala ya kutumia kampeni kumshambulia Magufuli.

Alisema ili kuondokana na hali hiyo, katika Bunge lijalo atapendekeza Sheria ya Uchaguzi ibadilishwe ili kuthibiti vyama vinavyoacha kunadi sera na kushambulia wengine.

"Haiwezekani kuwa na mtu muda wote analalamika tu, mimi nilikuwa na Lissu (Tundu) bungeni hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndio maana nilikuwa namuita Malalamiko FC, kimekuwa chama cha malalamiko na kuzungumza kashfa na kejeli.” alisema na kuongeza;

"Wana bahati mwaka huu Mwenyekiti wetu (Rais Magufuli) ametukataza kuzungumza kashfa wakati wa kampeni. Nilikuwa nimeagiza kontena tatu hivi na zilikuwa zimefika bandarini, shughuli ingekuwa nzito, wamshukuru Rais Magufuli alivyowabeba amekemea hataki kampeni za matusi wala kashfa, lakini tunavumilia inafika mahali tutashindwa."alisema Lusinde.

Alisema Lissu alishambuliwa na linajulikana, ila si sahihi kusema serikali ilihusika na ameliomba Jeshi la Polisi limtafute muhusika ili serikali isiendelee kuchafuliwa.

"Pia Lissu amekuwa akiziimba risasi 16 je ndio ilani?, anasema wananchi wanahofu, mbona yeye tangu afike hapa nchini hatujamuona akiwa na barakoa na anatembea kila mahali bila hofu na kwa uhuru, sasa hiyo hofu ya kwa wananchi iko wapi? aache uongo na azungumzie sera kama wanazo,"alisema Lusinde.

Alisema Rais Magufuli amejipambanua kuwa ni mwadilifu na mzalendo mwenye lengo la kuifanya Tanzania kupiga hatua za maendeleo huku akifanya kampeni kistaarabu bila kumshambulia mtu na kuomba kura kwa watu wote.

"Ameomba kura hadi upinzani wamchague, hajambagua mtu, hajashambulia mtu, muda wote anapambana kuhakikisha anapata ushindi wake na chama chake ili kuendelea kuwatumikia wananchi katika miaka mitano mingine,"alisema.

Kuhusu mgombea wa nafasi ya urais wa Tanzania kwa chama cha ACT Wazalendo, Bernad Membe mgombea Lusinde alimshangaa kuendelea kupiga kampeni muda mrefu katika mkoa mmoja na kusema wagombea kama hao wanapoteza muda na kuitia nchi hasara.

"Wakati mgombea wa CCM, Rais John Magufuli akiwa amefikisha mikoa tisa kwenye kampeni zake na kukanyanga kiatu kweli kweli, mgombea wa ACT-Wazalendo bado yuko Lindi, sijui anagombea urais wa Lindi au wa kijiji cha Londo, baadaye hawa wagombea watapiga kelele kuwa wameibiwa kura, nataka Watanzania walione hili mapema."alisema Lusinde.

Alisema Mkoa wa Dodoma umeamua kura zote apewe Rais Magufuli kutokana na kuibadilisha sana jiji hilo. "Tunataka kuvunja rekodi ya kumpa ushindi wa kishindo Magufuli ili awe na deni kwa Watanzania litakalomfanya apige kazi kwa kiwango cha kutisha nchi isonge mbele. Magufuli sio mtu wa kusafiri nje ya nchi, lakini ameweza kuibadili nchi kwa kiwango kikubwa na kuifanya maeneo mengi yanafanana na nchi za nje."alisema.
 
Chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, na hiyo 28 oct ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Mkuu kumbe Hilo unalijua hata wewe.

Unaona je ukiandika waraka kwa chadema kuwashauri wasitishe Kampeni zao njiani ili wasiendelee kupoteza HP za mwili angali mshindi anajulikana.
 
Mkitaka msitake mwaka huu mnaondolewa na nina wasiwasi hata polisi na majeshi wameshawachoka huwenda kazi ikawa rahisi zaidi kama mtasubutu kuvuruga uchaguzi kwa kutaka kujitwalia madaraka bila kupingwa au kupigiwa kura.
 
Mmeanza kuweweseka hata wiki mbili za kampeni hazijaisha
Tutawatandika kipigo cha mbwa mwizi huu Uchaguzi
Chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, na hiyo 28 oct ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Hatuwezi kususia Nchi wahuni tumewapa miezi miwili ya kuropoka

Baada ya October nidhamu itawale na yule jamaa enu arudi ubeliginyi[emoji3]
Mtasema yote atumike na mabeberu au wahisani na wadau wa maendeleo sisi tunachotaka msuse kabisa kufanya kampeni maana msumari umeingia mahala pake.
 
Kazi nyepesi Sana mwaka huu kwa jinsi Magufuli anavyobweka Sasa hv Hali ni tete Sana sana
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli...
Wakati ukuta sasahivi anaongelea maendeleo
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli...
Lusinde kibajaji anajipendekeza kwa mtukufu ili awamuru NECCCM Tumeccm waanze kutembea na matokeo yake mfuko tarehe 28 wapore jimbo la mtera kwa njia haramu za kishetani, huko jimboni kwake wanalalamika haoengelei maendeleo Bungeni bali yeye kawa mwimba taarabu mda wote ni mipasho umbea hana anachokiwaza cha maana.

Tundu lisu ni Mwanasheria lazima alalamike mda wote kwa sababu Serikali ya CCM haitendi haki imezidisha uonevu unyanyasaji na mambo mengi ya kishetani.
 
Hivi tumekosa hoja za kujadili kiasi cha kupoteza muda kujadili porojo za akina Ludinde? Lusinde I believe is one of the very low mind parliamentarians.

Hana elimu wala maarifa wala kiwango cha kawaida cha IQ. Ni mtu wa porojo nyingi kama walivyo wengi wasio na uelewa wanaotaka kuziba mapungufu yao ya uwezo wa kufikiri kwa kuongea sana, japo wanachoongea huwa hakina maana.

Spika wa Bunge aliwahi kutamka kuwa TL alilisaidia sana Bunge katika kutunga sheria. Mambo ambayo walikuwa wanategemea yafafanuliwe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni Lisu ndiye alikuwa akifanya kazi hiyo.

Hivi Spika Makinda na Lusinde - nani mwenye uelewa zaidi? Tujadili hoja zinazotolewa na watu wenye akili timamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…