Lusubilo Mwakibibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, huyu ni adui namba moja wa demokrasia nchini

Lusubilo Mwakibibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, huyu ni adui namba moja wa demokrasia nchini

Marangu

New Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
1
Reaction score
0
lusubilo Mwakibibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, huyu ni adui namba moja wa demokrasia nchini. Ameshiriki katika matukio mengi sana ya kuchezea uchaguzi na anaweza kuitwa mchochezi, mhaini anayetaka kuvuruga amani ya nchi yetu kwasababu ya kujipendekeza na kutumika na Chama tawala.

Tunafahamu ni mtu mkubwa huko kitengoni Makumbusho, lakini hii isiwe sababu ya kutumika kuvuruga mshikamano na hatima ya nchi yetu kwa kutumikia zaidi chama tawala. Mama tunaomba huyu mtu aondolewe haraka sana maana hajui maana ya demokrasia yeye anachojua ni CCM lazima washinde. Watu kama hawa ndio wataendelea kutumikia zaidi chama kuliko watanzania.

Alianza huu mchezo huo Kakonko akiwa DED katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma, uliofanyika August 2018 ambapo mgombea wa CCM Profesa Christopher Chiza, alitangazwa mshindi kwa kushinda kwa kura 24,578 huku mpinzani wake Elia Michael wa CHADEMA akipata kura 16,890. Uchaguzi ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Chadema Mwalimu Kasuku Bilago kufariki dunia Mei 2018. Lakini nwote tunajua aliyeshinda alikuwa ni mgombea wa CHADEMA lakini kwa kutumia ubabe, umafia, dola na nguvu za ushushu meza ikapinduliwa Chiza akatangazwa mshindi na huyu Mwakibibi.

Kwa kazi hii hii chafu akapewa promosheni na kuhamishiwa Temeke, ambako alikutana tena na uchaguzi wa marudio baada ya mbunge wa CUF Abdalalh Mtolea kuhamia CCM , na baadaye kugombea kupitia CCM. Inaeleweka kitendo cha Mtolea kuhamia CCM kiliwaudhi sana wana Temeke na waliahidi wazi wazi kuwa hatapata kura zaidi ya 20. Baada ya kuliona hilo Mkurugenzi Mwakibibi kwa mara nyingine tena aliamua kutumia tena umafia na kumwekea mizengwe kipenzi cha wana Temeke mgombea wa CUF ambaye alitiwa misuko suko hadi ikaonekana kama ameamua kusarenda kugombea na Mtolea akapita bila kupingwa. Kwa mara nyingine tena, huyu jamaa alitumia madaraka yake kuvuruga uchaguzi kwa maslahi yake binafsi na kukitumia tena chama cha mapinduzi.

Kufika mwaka 2019 na mwaka 2020, huyu jamaa akawa amelewa sifa na kujitapa hadharani kuwa mahali popote atakapokuwa msimamizi wa uchaguzi hakuna chama kitashinda zaidi ya CCM. Hata ikitokea uchaguzi ukafanyika Marekani yeye anajua kuchezesha mchezo huo. Ni kweli uchaguzi wa seriakali za mitaa tuliona jinsi yeye mwenyewe alivyokuwa anavuruga uchaguzi kuhakikisha CCM wanashinda

Hata uchaguzi wa Rais wilaya ya Temeke ndio wilaya ambayo CCM na Rais JPM walipata kura zaidi kuliko wilaya yoyote Tanzania. Yote haya tunajua ni kwasababu ya faulo zake huyu jamaa. Aliandaa mkutano mkubwa wa kampeni Temeke ili kujipendekeza kwa Chama. Kimsingi huyu jamaa ni mtumishi wa Chama Zaidi kuliko serikali. Yeye kwake CCM ndio namba moja kuliko serikali

Maumivu aliyowaachia wana Temeke na watanzania ni makubwa sana, na kama Mungu yupo atajibu maombi maana yule kivuruge mwingine wa Kinondoni Aaron Kagurumjuli aliyekuwa mkurugenzi wa Kinondoni alishaondolewa katika mazingira ambayo hata aliyemuondoa alikuwa haelewi, na mpaka leo hakuna anayeamini kama kaondoka kweli, kumbe ulikuwa ni mkono wa Bwana uliwapiga upofu wakamuondoa licha ya kuwa siku zote alikibeba chama cha mapinduzi, malipo ni hapa hapa.

Tunaomba sana huo mkono wa Bwana, ugeuke na uwapige upofu ili huyu kivuruge mwingine aondolewe kama mwenzie wa kinondoni kwa kukosa la kupindisha haki na demokrasia.

Siku za karibuni ameonekana kama ana wasiwasi fulani, nadhani hana uhakika na hatima yake, na akitumbuliwa ataweka wapi uso wake kwa zile rafu alizocheza kuanzia Buyungu hadi chaguzi hizi tatu yaani marudio 2018, serikali za mtaa, na wabunge na rais 2020. Ni wakati wake wa kulipa malipo ya kutumia ofisi za umma kutumikia CCM.

Wakati wa kulipwa umefika ajiandae kwenda kuungana na Kaju kada mwingine wa CCMaliyetumia ofisiza serikali kuendesha siasa za chama tawala
 
Back
Top Bottom