Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Lutgard Kagaruki, akizungumzia kumbukumbu zake za Oktoba 29, ameeleza masikitiko yake kuhusu taarifa za kupotea kwa miili ya watu.
Amesema, “Tukasikia miili ya marehemu imepotea. Niliona taarifa za wahusika wakizika nguo na viatu. Kuna mambo mengi ambayo bado hatuyajui. Miili iliyopotea ilipelekwa wapi? Wengine wanasema ilizikwa kwenye makaburi ya jumla, lakini hatujui ilipo.”