Lwakatare amefutiwa mashtaka ya ugaidi kutokana na mmoja wa mawakili wake kuwa mbunge?

Lwakatare amefutiwa mashtaka ya ugaidi kutokana na mmoja wa mawakili wake kuwa mbunge?

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,895
Reaction score
20,392
Kuna hali ya sintofahamu juu ya WILFRED LWAKATARE kufutiwa mashtaka ya UGAIDI huku wengi wakiamini kuwa maamuzi hayo ya mahakama yametokana na ukweli kwamba suala hilo lilitawala mijadala ya bunge linaloendelea DODOMA na kwa maana hiyo Mahakama haikuwa na namna nyingine hasa ukizingatia kuwa mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi ni alikuwa Mbunge.

Mytake:kama maoni haya ya watu ni ya kweli, basi ni dhahiri kuwa sasa wananchi watakosa mahali pa kupatia haki zao.napendekeza kwenye Katiba mpya kiwepo kipengele cha kutomruhusu mbunge kuwa wakili katika kesi zenye maslahi kwa taifa.
 
Mlimfanyia dr.Lamwai vitimbi mpaka akatoka udsm kama lecturer na mwana chadema,akaja ccm mkamtumia kama toilet paper,sasa mnakuja na hili la mbunge asiwe wakili
 
Magaidi waliopo duniani kwasasa wote dini yao inaeleweka, hakuna gaidi Mkatoriki, watu wasipotoshe maana. Lwakatere kasingiziwa.
 
Kwani anayefuta mashitaka ni wakili au hakimu? Hivi mtu anahitaji kuwa na shahada ya sheria kufahamu kwamba mashitaka yalikolezwa chumvi?! Wewe ushawahi kusikia magaidi wanateka mtu?
 
Kwani anayefuta mashitaka ni wakili au hakimu? Hivi mtu anahitaji kuwa na shahada ya sheria kufahamu kwamba mashitaka yalikolezwa chumvi?! Wewe ushawahi kusikia magaidi wanateka mtu?

Unahangaika nini na huyo jicho,yupo katika kuongeza thread ili idadi itimie akadake 7000 yake. Njaa sio kitu kizuri asilani,unawezajifanya chizi ili ule...
 
Kuna hali ya sintofahamu juu ya WILFRED LWAKATARE kufutiwa mashtaka ya UGAIDI huku wengi wakiamini kuwa maamuzi hayo ya mahakama yametokana na ukweli kwamba suala hilo lilitawala mijadala ya bunge linaloendelea DODOMA na kwa maana hiyo Mahakama haikuwa na namna nyingine hasa ukizingatia kuwa mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi ni alikuwa Mbunge.

Mytake:kama maoni haya ya watu ni ya kweli, basi ni dhahiri kuwa sasa wananchi watakosa mahali pa kupatia haki zao.napendekeza kwenye Katiba mpya kiwepo kipengele cha kutomruhusu mbunge kuwa wakili katika kesi zenye maslahi kwa taifa.

Una tatizo la kutumia ubongo wako. Ufafanuzi wa kesi hii ulitolewa hatua kwa hatua, hilo la wakili kuwa mbunge only shallow skills discussing that.
 
Hoja yako ni ya kijinga na unaonekana uwezo wako wa kufikiri na kuchanganua mambo ni mdogo sana.Kwa kuwa asiyejua maana haambiwi maana basi baki na ujinga wako kwa kuwa unakulipa kupitia 7,000tsh za Lumumba.
 
Siwezi kushangaa mawazo mgando ya huyu bwana maana Tanzania bado tuna adui ujinga, shitaka la ugaidi ni endapo kikao cha kigaidi kimejumuisha Watu zaidi ya watatu na Jalapa la kesi limewashitaki Watu wawili tu, hivyo kupoteza sifa za kigaidi.
 
Mahakama haikuwa na namna nyingine hasa ukizingatia kuwa mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi ni alikuwa Mbunge.

wakili wake ni mbunge?

Mbona mmoja wa watengeneza movie hiyo ni mbunge
 
TanguLini kesi iliyo mahakamani ikaongelewa bungeni, na kwanini ilikubaliwa?
Je ndg Lukuvi alikuwa likizo wakati huo?
 
Mlimfanyia drLamwai vitimbi akatoka udsm kama lecturer na mwana chadema akaja ccm mkamtumia kama toilet paper,sasa mnakuja na hili la mbunge asiwe wakili

....Kweli Dr Lamwai walimtumia kama big G then wakamtema!
 
Ni kwamba hana hatia...usilete siasa-gamba hapa, kesi ya kuchonga haiwezi kuwa na nguvu mahakamani, pia wanasheria wanazifaham sheria, ndio maana magamba chali...teh..teh...maccm ni ya ajab kabisa
 
Back
Top Bottom