Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mtu pekee ambae bila shaka umma una hamu ya kusikia kauli yake kuhusu ukweli wa ile video ambayo baadhi wamedai ni fake na wengine kudai ni ya kweli ni Lwakatare mwenyewe.
Maelezo ya nini kilitokea na ilikuwaje akaonekana kwenye hiyo video kutoka kwenye kinywa chake kitatusaidia kubaini ukweli hasa wa nini kilitokea.Japokuwa nae ni mtuhumiwa na kwa vyovyote vile ataeleza kwa namna ya kujilinda ila kwa kuzingatia taarifa zilizopo mpaka sasa kuhusu swala hili na ukweli kuwa wengi wetu tumeshuhudia hiyo video basi vyovyote vike atakavyoongea itakuwa ni swala la sisi kuunganisha dots tu kupata ukweli wa ni nini hasa kilitilokea.
Tumeshasikia na kusoma mengi juu ya jambo hili,kuanzia kauli za wanasiasa na watu wengine wakiwemo wataalam wa video,mtu pekee na pengine muhimu kuliko wote ni Lwakatare mwenyewe.Kauli ya Lwakatare,kwa vyovyote vile,itajibu maswali yaliyomo vichwani mwetu kuhusu tukio hili ambao wengi tunaliona ni kama mchezo wa kuigiza.
Sasa swali,Je, iwapo ataachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kwa mara ya pili ataruhusiwa kuongelea jambo hilo?Au ndio itakuwa kama kawaida kwamba kesi iko mahakamani na hivyo jambo hiliol haliwezi kujadiliwa popote pale au hata kulitolea taarifa yoyote ile?
Wataalamu wa sheria mtusaidie ni nini Lwakatare anachoweza kufanya na nini haruhusiwa kukifanya kwa sasa endapo atapata dhamana.