....Hata hivyo, haya maandamano ni changamoto kubwa kwa CUF. Maana walipomtema kwenye uongozi kiaina sidhani kama walijua nguvu yake huku Bukoba. Kimsingi Lwakatare ni nguzo nzito sana ya CUF huku bara, kiasi kwamba akinyanyua mguu akautua kwingine atakuwa ameisambaratisha kabisa nguvu ya CUF huku. If I were to be a devil's advocate, can we sustain two strong opposition political parties in TZ? Kwa kuwa ushirikiano umeshindikana, wanasiasa mahiri lazima waamue uwanja wao kufanya siasa-ama CHADEMA au CUF. Kwa maoni yangu sioni kwa nini Lwakatare aendelee kubaki huko alipo. Kimsingi hana sababu!