There is more than meets the eye. Leave George alone. He is doing his job. So far not bad at all. If you have personal grudges against George, be advised to save them for another day.
Did you attend the game against Ndanda yesterday? Do you expect Lwandamina to enter the field and play? How many clear chances were missed?
The league is not even halfway. We are struggling to pay wages, yet you want George fired and paid the severance package. Hiring a new coach will also need money. Are you going to contribute a dime?
Kwa kuwa wewe ni mwenzangu tuongee kwa lugha ya kwetu. Umeziona mechi za lipuli na njombe mji. Uliona uwezo wa wachezaji pale ilipotakiwa kutafuta point. Umeziona mechi za Yanga, tunaposhinda ni kwa shida na goli moja. Mechi zote ni goli moja moja. Unamaanisha hatuna watu wanaoweza kufunga hadi Msuva arudi?
Umeiona mechi ya jana, Ngoma amecheza zaidi ya dakika 20 akiwa ameumia na kujivuta na kocha anamwacha mpaka dakika ya 90 ndo anafanya sub. Ngoma karudi juzi toka kuumwa, unamwona anachechemea tena na kiwango kiko chini kwanini usifanye cha kuisaidia timu kwa haraka zaidi
Mwangalie kocha na benchi lake, toka dakika ya 1 hadi ya 90 wamekaa chini kana kwamba wanaumwa, msaidizi wake vile vile. Kisaikolojia, kocha kusimama na kusisitiza katika mchezo ina faida kubwa sana na mifano ningekupa mingi tu ila kwa leo nakupa ule wa mwaka jana wakati Ureno wanashinda kombe la Ulaya kwa kuwatoa wafaransa. Ulimwona Ronaldo na kocha na benchi zima walivyosimama kuwahamasisha wenzao hadi wakaweza kuishinda ufaransa iliyokuwa bora kuizidi Ureno kwa mambo mengi.
Tunataka kujua, Lwandamila akiwa Zesco timu yake ilikuwa inaweza kushinda magoli mangapi kwa mchezo mpaka anakuwa bingwa. Na ni kwanini hapa inamwia vigumu? Unaweza ukasema ligi ni ngumu, sawa. Lakini mbona wengine wanafunga zaidi ya magoli 2 na kuendelea kuliko ilivyo kwa Yanga. Hata jana Majimaji kampiga Mwadui tena kwake, Mtibwa na akina Singida U wanaweza kufunga kuliko sisi katika mechi nne. Ni kweli wa kwetu uwezo ni mdogo kuliko wale? Mbali ya kufundisha, kocha ni mtu wa kuzalisha hamasa na kuwajenga wachezaji hata kama kuna magumu vipi. Ukocha ni art.
Kwani kipindi cha nyuma si wachezaji waliwahi kuwa wanacheza bila malipo, lakini mbona walau kiwango kilikuwa kikionekana? Na kuna hata kipindi timu ilikuwa ikifungwa lakini kimchezo timu ilibaki kuonekana inacheza vizuri sana. Mchezo wa jana umekuwa ni mbovu kuliko kwa miaka zaidi ya 7 iliyopita. Na kama hakifanyiki kitu kwa haraka basi ilimradi wa kutetea mpo basi endeleeni kutetea, lakini repurcusion ipo na mtaipata. Mwangwi mtausikia tu kutoka nje
Kwa kumaliza nakuomba uangalie tena mashabiki wa Yanga jana uwanjani. Kama unaweza ukasoma saikolojia zao basi waambie wenzio ipo siku uwanjani timu itaingia na haitakuja kuwa na mashabiki wake. Kwanza wamepoa sana na hata goli lilipofungwa bado hawakuonekana kukubali lakini pia angalia idadi yao kwa haraka. Unaweza ukasema uchumi mbaya lakini ntakuuliza mbona Simba wanajaa uwanjani? Wao ndo hawaguswi na uchumi?
Mficha uchi .....