Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Dar es Salaam. Kocha Mzambia George Lwandamina anatarajia kutua Yanga baada ya safari yake kuiva kufuatia mwajiri wake, Kampuni ya Umeme Zambia (Zesco) kukubali kumuachia.
Habari zilizopatikana zimeeleza kuwa Yanga ilimtumia tiketi ya ndege kocha Lwandamina na usiku wa kuamkia leo alitarajiwa kutua nchini.
Uongozi wa Zesco United, ulithibitisha kuachana rasmi na kocha huyo ambaye pia ni kocha wa muda wa timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo.
“Zesco United inapenda kuchukua fursa hii kutangaza kuwa kocha wake mkuu George Lwandamina asubuhi ya leo, (jana) ameamua kujiuzulu kwa sababu zisizozuilika.
“Klabu imekubaliana na maombi yake ya kujiuzulu, inapenda kumshukuru kwa kazi na mchango wake mkubwa katika kipindi chote alichokuwapo kwenye timu.
“Tunapenda kuchukua nafasi hii kumtakia Lwandamina, mafanikio katika safari yake,” imesema taarifa ya klabu hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, Justin Mumba.
Mpaka sasa Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 30 baada ya michezo 14 ikisubiri mchezo wa mwisho na Ruvu Shooting. Simba ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 35 na inacheza na mechi yake ya mwisho na Prisons mjini Mbeya.
Chanzo: Mwananchi