Jangakuu
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 513
- 221
Katiba ijayo inatakiwa isiwe na lugha za ulaghai, iamue na kuelekeza nani afanywe nini kama atavunja sheria za nchi na itamke wazi uelekeo wa uchumi wetu."Haya ni maelezo ya Mwasisi wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Leo Lwekamwa, anapozungumzia Mchakato wa Katiba na hatima ya Tanzania.
Lwekamwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kwanza wa chama hicho cha upinzani, kilichojizolea umaarufu mkubwa wakati wa uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi nchini, anasema rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi chini ya mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, haina tofauti na katiba iliyopo katika baadhi ya maeneo.
Hata hivyo anaipongeza Tume ya Katiba akieleza kuwa imefanya kazi kubwa nzuri ila bado haijaja na hatima ya taifa na Watanzania katika mambo kadhaa.
Anasema rasimu hiyo haijatofautiana na katiba iliyopo katika baadhi ya maeneo. Kinachoonekana kimantiki na kimaamuzi baadhi ya mambo bado yaleyale, anasema.
Anaeleza muuundo wa Mahakama bado umeminywa kwa Jaji Mkuu na Naibu wake kuteuliwa na rais kisha kudhibitishwa na Bunge. Kiufanisi, jambo hilo halina mabadiliko yoyote.
"Rais anawateuwa na kuwapeleka bungeni, je huko bungeni kama idadi kubwa ya wabunge itakuwa ni wa chama kitakachokuwa kinatawala huoni watapitisha majina hata ya watu wao," anahoji Lwekamwa na kuongeza:
"Jaji Mkuu anatakiwa kupatikana kupitia jopo la (TLS) Chama cha Wanasheria wa Tanganyika ambao watasimamia mchakato mzima na akipatikana kwa mfumo huu utamfanya kutenda haki bila kizuizi chochote."
Mwasisi huyo wa TLP aliyekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2005 anasema, kunatakiwa kuwapo kwa Tume ya Kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma inayojitegemea na yenye kufanya maamuzi pasipo shinikizo kutoka sehemu yeyote.
"Tume inakuwa inajua kila kitu, unakuta mtu anaingia madarakani hana hata baiskeli, lakini kwa kipindi fulani anakuwa na mali nyingi. Kitendo cha tume kutokuwa na meno kinafanya viongozi hao wasichukuliwe hatua yeyote," anasema na kuongeza;
"…Tume inatakiwa kuongezewa meno ya kuwashitaki katika Mahakama ya Katiba vingozi hao, ambayo nayo inatakiwa kuanzishwa ili wale wote watakaokuwa wakibainika kuhujumu mali ya umma wachukuliwe hatua kali na za kinidhamu."
Anasema katiba kama haijasema kuwapeleka mahakamani, Bunge halitatunga sheria hiyo, kwani wabunge wa chama kitakachokuwa madarakani wanaweza kuwa wanawafahamu wezi na hivyo kutaka kuwalinda
Kuhusu muundo wa Bunge Lwekamwa anasema, bado kuna upungufu kutokana na Kiti cha Spika na Naibu wake, kubaki kwa chama kitakachokuwa na wabunge wengi bungeni.
"Kusema kwamba wasiwe Wabunge wala wanasiasa ndani ya miaka mitano nyuma si sahihi, kwani Serikali ndio inayowajua. Mfano Maofisa wa Polisi au Jeshi hawa si wanasiasa, lakini wanapostaafu katika nyadhifa hizo utawasikia wanagombea nafasi za kisiasa," anasema Lwekamwa na kuongeza:
"Njia sahihi ya kuhakikisha kiti hicho kinatenda haki na kusimamia chombo hicho muhimu ni Spika na Naibu wake kutoka kwa mshindi wa pili wa tiketi ya Urais yaani upinzani. Hapo ndipo usawa utakuwepo, tofauti na hapo bado hakuna lolote litakalofanyika."
Akifafanua kuhusu viti maalumu na ukomo wa ubunge anasema, kuviua viti maalumu ni janga kutokana na umuhimu wake, lakini kuviondoa ni kuongeza gharama kwa kufanya kila jimbo kuwa na wagombea wawili; mwanamke na mwanaume.
"Tuviache viti maalumu na ukomo wa ubunge uwe awamu mbili, lakini tatu bado ni nyingi sana kwani wakati mwingine inakuwa kero," anaeleza.
Akielezea Muundo wa Muungano anasema, Tume inayosimamia Mchakato huo imefanya vizuri kupendekeza Serikali tatu ila akataka Serikali iwe ya Tanganyika, badala ya Tanzania bara.
Kuhusu Tume ya Uchaguzi, anaeleza kuwa ni moja ya vitu ambavyo vikikosewa, vinaweza kuleta amani au kuivunja kutokana na kutokutenda haki kama wananchi wanavyotarajia.
Anasema licha ya kwamba itakuwa Tume Huru ya Uchaguzi na imeongezewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, bado haitakiwi viongozi wake na wajumbe kuteuliwa na Rais.
"Tume isiundwe na Rais, watu waandike barua na waombe na wahojiwe na kamati huru ya wataalamu kutoka vyombo vya dini, Wasomi, TLS pamoja na wawakilishi wa Vyama vya," anasema Lwekamwa.
Anawabainisha viongozi hao kuwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Msajili wa Vyama ambao Rais asihusike kwa lolote kupatikana kwao.