Ni biashara nzuri sana kama ukiweza kuijua vizuri' nasema nzuri kwasababu unadeal na pesa mda wowote na unaweza kutumia mtaji mdogo na kupata faida robotatu ya mtaji ulioweka' kwahiyo faida ni zaidi ya nusu ya mtaji wako, hivyo miezi miwili unakuwa ushaweka pembeni mtaji ulionzia. binafsi naifanya na kwakweli si haba ukilinganisha na kimshara nilichokuwa nalipwa enzi nimeajiriwa.
Kwanza unapofikilia biashara lazima uwe risk taker! Tofauti na hivyo biashara hautofanya. Nasema hivyo kwasababu naona unatangulia kuuliza changamoto' badala ya kuuliza vigezo vyakuupata uwakala'. Changamoto kubwa kwenye biashara hii ni ;
1) utapeli, ujambazi ( watu waweza kuja na bastola, kukuletea hela feki, kutoa pesa hewa)
2) Eneo la biashara na mzunguko wa pesa au biashara katika eneo husika
3) huduma Kwa wateja
Swala mtaji haina kiwango maalum' itategemea unakusudia kuingiza faida gani? Eneo ulilopo mzunguko wake kwa hiyo biashara upoje?
Swala la faida pia linategemea sana uwingi wa wateja wako! Kuna viwango vya commission kwakila transaction. Hivyo commission kwa muamala inaanzia tsh 40 - 2500 transaction. Kwa commission hizo kuna watu wanaingiza faida 5000 Kwa mwezi Kwa mtandao mmoja lakini pia kuna watu wanaingiza zaidi ya 1,500,000 tsh kwa mtandao mmoja. Hivyo huyo mtu anaeungiza 5000 kwa mtandao mmoja ukijumlisha kwamitandao yote mitatu yaani tigo, voda, aitel anawastani wa 15,000 au yaweza zidi au kupungua kidogo. Huyo wa tsh 1,500,000 times 3 sawa na tsh 4,500,000 inaweza pungua au kuongezeka kidogo.
Nimeandika kimazabemazabe kidogo' kwahiyo naweza nisieleke vizuri hivyo nakaribisha maswali maana hizo ndio shughuli zangu hapa mjini.