M-pesa, tigo Pesa, airtel Money na Maangamizo ya Uchumi wa Tanzania


Hakuna bank hapa nchini mkuu! kabda kama unaishi ughaibuni

hakuna reliable huduma za m pesa pia!! wizi na uongo mwingi

hakuna serikali pia! LOL!
 

Wewe umesahau simplicity na urahisi wa huduma hizi kwa wananchi amabo kuaccess huduma za kibenki ni ndoto. Hebu fikiria jinis ilivyokuwa rahihi kuwatumia fedha wazazi vijijini, watoto shuleni, wafanyakazi mashambani n.k all this contributes positively kweny uchumi wa nchi
 
Nimejaribu kusoma ujumbe wako ila sijakuelewa vizuri...Labda upunguze hoja katika para moja na ujaribu kufafanua issue moja moja.

Mfano, bank gani hapa nchini zinatoa riba kwa saving accounts ambazo ndiyo wengi wetu tunazotumia?

Babu DC!

Mkuu hata kama hazitoi riba ila pindi ile hela yako inapokwa bank
inaweza akatolewa kama mkopo ktk secta mbalimbali za uzalishaji
ambazo zitachangia ktk kipato cha taifa pamoja na ukuaji wa uchumii
la inapokuwa ktk M pesa au togo pesa haiwezi kukopeshwa na kufanya
uzalishaji kama unaofanywa na bank ambao ndo kasema kuweka hela
kwenye hiyo mitandao ni sawa na kuichimbia chini
 

Mkuu embu ongelea ktk upande wa uchumi ina madhara gani?
 
Hizi ndizo kero za Mabenki yetu.

1. Process ya kufungua account katika baadhi ya mabenki yetu ndefi.
2. mlolongo wa documents, lete barua kutoka kwa ofisi za serikali za mitaa, n.k
3. amount ya kufungulia account ipo juu hadi 50,000,
4. Huweza ku-access account yako muda wote.
5. Gharama kubwa za uendeshaji akaunti (maintance fee)

lakini mpesa ni kitambulisho chako tu. mabenki wanapaswa kuboresha huduma zao, imekula kwao. HEKO MPESA,Tigo PESA, Airtel Money.
 
aise ni same things walau hata hao m pesa na tipo pesa wanakwambia wanachukua kiasi gani. Shenzy mabenki kwa maskini tunaibiwa wala haizai na afadhali uichimbie chini utakuta pesa haijapungua. Benki kama una laki mbili tatu kaa mwaka uone pesa inauvyopungua kingine kinaogopesha wananchi hicho. Hawa elektronic money m pesa tigo pesa wanakwambia wazi
 
Sasa hivi huduma za Mpesa, tigopesa nk zinaratibiwa na BoT. Nadhani kuna kiasi ambacho wametakiwa kukihifadhi BoT kama inavyofanyika kwa mabenki...
Benki zilikuwa na miaka mingi ya kuwafikia wananchi wote kwa kipindi tangu nchi ipate uhuru mpaka hivi karibuni kulipoanza hizi M pesa nk lakini hazikufanya hivyo. Mpaka mwaka 2008, wateja binafsi waliokuwa na akaunti benki walikuwa hawazidi laki tano katika nchi yenye wananchi milion 36 by then. So benki wajilaumu wao wenyewe... Walikuwa na nafasi ambayo hawakupenda kuitumia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…