M-PESA.TIGO PESA na MAHUSIANO...

Hivi wakuu hakuna line isiyo na huu ujinga ujinga wa dash dash PESA ili niwe nasema line yangu haitumagi hela??????????????
 
Nyie nanyi mnanishangaza. . .
Unafikiria jibu la kumjibu wakati tayari jibu liko wazi?Mwambie huna. . .ebooo!!! Wanaume wazima mnakua kama wavulana bana, au ni wavulana?
 
mmh mie maisha yangu yamekuwa marahisi haswa na izi huduma kwangu nying faida si hasara ,
wadhamini kibao yan duuh! ki ukweli wanajigonga wenyewe mie sikatai tuma baba!
 
Hivi wakuu hakuna line isiyo na huu ujinga ujinga wa dash dash PESA ili niwe nasema line yangu haitumagi hela??????????????
teh kwani anakulazimisha yan kujisumbua si unasema tu sitaki au sina!
tatizo mnapenda kujikweza ivyo tutumieni tu sie tunapokea.
kizuri ni kwamba ww mwenyewe unaenda kunitumia lolz, kwa mapenzi yako! coz nikiomba sio lazima unipe na wengi wenu mnajiongezaga wenyewe bana.
 
Ukikitumia kitu vibaya lazima upate athari zake....btw Boss naomba umwambie Lily Flower hapo chini namsalimia sana..muulize kama ana M PESA nimtumie hela ya kununua mchicha nasikia siku hizi umepanda bei fungu linauzwa buku...

Mkuu....choooonde... kibubu chetu usikivunjage...
 

Ha..ha..ha Kumbe ndio majina tunayopachikwa haya.M-pesa Man!! dah umeniacha hoi.Most women deserve an Oscar when it comes to this act.
 
lolz! hii mitandao ina umuhimu wake jaman, kama unaitumia vibaya sawa utajuta tu siku zote.
mie tangu haya makitu yaweintroduced dah maisha yangu yamekuwa marahisi mara 200 lolz.
tanx to founders wa haya mambo aisee, well done guyz.
 
Hahahaaa nicheke kwa afya yangu mie. . Ukizaliwa mwanaume tabu kwelikweli mie hata nilikuwa sijawaza eti kuna watu hii huduma imekuwa kero kwao lol. .ukiona mwanaume anasoma msg anakuna kichwa saivi si bure anatafuta jibu. .No network. .Lol lol. .
 
hii mitandao ya simu pesa imesaidia sana kwa wale ambao wana adabu au wanaiheshimu matumizi yake , kwani kwanza imerahisisha ukaribu wa kutuma na kupokea pesa hasa unapokuwa umekwama au umepata tatizo ni rahisi sana kuliko hata banks ...
ila waleeee wengine ndo imekuwa ni sehemu ya kusumbua au kuleta usumbufu maana kila mara ninaomba nauli nitumie kwenye tigo pesa etc sasa ukikaa ukajiuliza hata ukimtumia buku na gharama zake ni ngapi na nini mantiki ya hilo haiji kichwani
 

tatizo lako wewe umeelewa angle moja tu
wenzio tunazungumzia angle zote
wala kutuma sio tatizo
wapo wanaofurahia pia kutuma na kuhonga kwa njia hii
na wanao hongwa ndo wanapata matatizo
tunazungumzia kwa ujumla wake
 
Ha..ha..ha Kumbe ndio majina tunayopachikwa haya.M-pesa Man!! dah umeniacha hoi.Most women deserve an Oscar when it comes to this act.

umeonaa ehh?
wewe umem save eti wife to be
yeye kaku save tigo pesa lol
 
huu ni ujumbe kwa wanaume
tugome kujiandikisha m pesa na tigo pesa
mimi siku zote hujibu 'bado sija register' niki register nitakutumia lol
mmmm, mtaweza? mnavyopenda kuonekana hamshindwi kitu! kumbe mnatuma huku mnaumia moyoni? ha haaaaa. kwa raha zenu!
 
tatizo lako wewe umeelewa angle moja tu
wenzio tunazungumzia angle zote
wala kutuma sio tatizo
wapo wanaofurahia pia kutuma na kuhonga kwa njia hii
na wanao hongwa ndo wanapata matatizo
tunazungumzia kwa ujumla wake

Ujumla gani??
Unless kuna watu wanatapeliwa/ibiwa bila wao kujua sioni lawama zinatokea wapi maana kwangu hayo mengine ni ya mtu kujitakia na kuendekeza.
 
mmmm, mtaweza? mnavyopenda kuonekana hamshindwi kitu! kumbe mnatuma huku mnaumia moyoni? ha haaaaa. kwa raha zenu!

sio wote tunaolalamika
usifikiri hapa ni malalamiko
tunaangalia athari kwa ujumla
 

You have said it all, Mkuu!!!

No more from me!!!!!
 
Ujumla gani??
Unless kuna watu wanatapeliwa/ibiwa bila wao kujua sioni lawama zinatokea wapi maana kwangu hayo mengine ni ya mtu kujitakia na kuendekeza.

watu wakisema mitandao ya jamii imeongeza watu ku cheat
hawalalamiki na kulaumu mitandao ya jamii
wanazungumza mabadiliko ya jamii yalioletwa na mitandao ya jamii
now umenielewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…