M- wekaeza Vs UTT

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Kuna wadau waliomba kujua toafuti ya M-wekeza, ipi bora , n.k
Nitaeleza kwa ufupi kwa wale wanaohitaji kupata hivyo visenti basi wanufaike.

UMILIKI
UTT AIMS nishirika la umma
M-wekeza ni mradi wa Vodacom na Sanlam ambayo ni mashirika ya kibinafsi

FAIDA NA HASARA
Faida ya M-wekeza ni hadi 13.% kwa mwaka japo kuna kipindi (siku) inaweza kiwa 12% kutegemeana na soko

Mfuko wa bond UTT una wastani wa faida ya 12% kwa mwaka na hutoa gawio kila mwisho wa mwezi . Compaund interest ya gawio hakuna.
Mfuko wa ukwasi unatoa faida 12% na inaweza kuzidi hapo lakini M-wekeza haizidi 13%

M-wekeza haina compound interest kwakuwa faida huwekwa kwenye mtaji tarehe 2-5 ya mwezi unaofuata. Lakini mfuko wa ukwasi na Bond faida huwekwa kila siku hivyo faida nayo inatengeneza faida.

Masuala ya usalama
Yote ni mifuko salama kwa kuwa inaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Labda nchi isambaratike ndio sijui nini kitatokea.

Usalama wa kibinafsi wewe mwenyewe.
Kwakuwa M-wekeza unaweza kutoa pesa muda wowote , ikiwa mtu ana namba yako ya siri anaweza kukuibia. Na pia wale wazee wa kubeti unaweza kushawishika kuchomoa huko unaleta kwa muhindi anakupiga , mara umenunua vocha. Kwahiyo hapa inahitaji nidhamu ya hali ya juu.

Mifuko ya UTT ukitaka kutoa pesa huchukua siku 2-5 za kazi kutegemea na mfuko hivyo sio rahisi fedha kutolewa hovyo

Mwisho. Biashara nibora zaidi
 
Ninachopendea UTT AMIS, kuuliza Salio ni bureee hata ukiuliza mara 10000 kwa siku bado ni Bure.
Pili, UTT AMIS ni ngumu mtu kukuibia pesa yako hata kama anaijua namba yako ya siri ya UTT.. kwani ukitoa hela UTT Iwe kwa simu(USSD), App au form lazima pesa itumwe kwenye account yako ya bank, kwa minajiri hii mwizi inabidi ajue namba zako zote za siri.. yaan ya UTT na bank
 
Darasa zuri

Hakika mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…