M2- DA- P reluctant to reveal info on what real happened the night mangwea died


Mrembo by Nature, nashukuru sana kwa elimu ulonipa leo maana nimepata mwanga wa kutosha ktk medani za kimataifa.

Aisee kwa mujibu wa hizo article ulizoni-direct nimewaonea huruma sana watu wa Hong Kong. Hii inatokana na wao kuwa kati ya mifumo miwili inayokinzana, yaani mfumo wa kibepari wa UK na mfumo wa kijamaa wa China. Na ukisoma kwa undani zaidi hizo article utagundua kua kwa sasa wa-Hong Kong wataendelea kuwa chini ya mifumo hiyo kwa muda wa miaka takribani 36 ijayo (kwa mujibu wa masharti yaliyomo kwenye Basic Law pamoja na Hong Kon hand over ya mwaka 1997).

Ukiingia kwa undani zaidi utakuta wa-Hong Kong wamechukua baadhi ya mambo mazuri toka mfumo wa kibepari na baadhi ya mambo mazuri toka mfumo wa kijamaa lakini pamoja na hayo hawataki kabisa kuwa chini ya China ambayo inakumbatia mfumo wa kijamaa wakati huohuo China nayo inaimendea Hong Kong ili kuirudisha ndani ya China.

Mkanganyiko unaongezeka nilipoona Hong Kong wanaamuliwa na Beijing kuhusu nani aitawale. Lakini uzuri uliopo kwa sasa ni kua Hong Kong inajitegemea ktk masuala ya kiutawala ya ndani kama sheria na mengineyo as Hong Kong ni Special Administrative Region (SAR) kama ilivyo Taiwan ila kikwazo ni pale inapotaka kutoka kumataifa lazima itumie China kama nchi.

Huruma zaidi inakuja pale itakapoisha hiyo miaka 50 iliyoainishwa na Basic Law (kwa sasa imebaki miaka 36) ambapo China (inayofuata mfumo kamili wa kijamaa ambao hautakiwi kabisa Hong Kong) itataka kuirejesha Hong Kong mikononi mwake na matokeo yake kuna uwezekano wa kuibuka mvutano kati ya Hong Kong na China kila mmoja akitetea matakwa yake, yaani Hong Kong itataka iwe na uhuru kamili kama nchi wakati huohuo China itataka kuirejesha mikononi mwake. Kazi ipo.

Sasa nimeelewa kwa nini binti kiziwi hakunyongwa ila kama angekamatiwa miji kama Beijing, Ghuanzhou, Tianjin au Shanghai basi kifo kingemhusu.

Kwa mara nyingine nasema asante sana Mrembo by Nature kwa elimu hii, yaani zamani nikajua Hong Kong ni mji unaomilikiwa na China moja kwa moja kumbe sivyo. Kweli nimepata mwanga wa kutosha.
 

Asante kwa shukrani, hata mimi mwanzoni nilijua hivyo, lakini asante kwa kukamatwa kwa binti kiziwi nimepata kujua hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…