chamilo nicolous
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 2,097
- 1,457
Unakosea Kumlaumu Uliyemsaidia kwa Kukusahau! Ni kweli kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha, pia ni kweli kuwa Kikulacho ki nguoni mwako! Tutasahauliana sana, watia Nia wezangu, 2025 tuliisubiri sana, sasa imefika!!!!!
Iko hivi, unaposahauliwa na mtu uliyemsaidia usikonde wala nini kwa sababu hata wewe unasaidiwa na watu ambao hukuwasaidia, umezaliwa na wazazi ambao hukuwazaa, unatibiwa na daktari ambaye hukumsomesha, utazikwa na watu ambao hutawazika.
Hii ina maana Gani? Ina maana kwamba tenda wema nenda zako, ukisubiri kubarikiwa na uliyemtendea wema utahuzunika sana maana hatakukumbuka, tena ukifuatilia vizuri utakuta huyo ndo anawatangazia watu kwamba huna akili!
Hujawahi kuona wanafunzi kibao wakifika vyuo vikuu wakiwaponda walimu wao wa sekondari na msingi kwamba hawana akili?
Sasa achana na habari za kwamba fulani nimembeba mgongoni lakini hanikumbuki. Ndiyo! Kwani wewe waliokubeba mgongoni na wewe uliwabeba?
Kuna kijana nilimpambania akapata kazi nzuri, tena akawa Mkuu wa kitengo, tena sekta nyeti hapa Tanzania. Siku moja tukakutana sehemu nyeti, akaniambia bro, siku ya kurudi nyumbani upite ofisini nifanye kitu, bila wewe nisingekuwa hapa. Nikasema sawa nitapita.
Basi siku ya kuondoka ilipowadia nikaanza safari ya kupita kwake, nilipofika katika mji wake alizima simu. Nikaondoka zangu.
Baada ya siku tatu akanipigia simu ameandaa maneno mengi ya kunipanga. Vijana wanasema alinipiga sound! Nikamwambia wala usijali dogo, MPAPAI HAULI MPAPAI YAKE!
Sikumlaumu wala kumshangaa maana hata mtu uliyemlisha mwaka mzima siku ikatokea mkakosa chakula, mkalala njaa, atakusema ulitaka kumuua. Fa masihara nini?
Mtu anamsahau mama yake mzazi sembuse wewe? Mzazi anasomesha mtoto kwa kujinyima mpaka anapata ajira, halafu mshahara wa kwanza anakwenda kula na demu wake! Iko hivyo!
Ndiyo maana huwa tunasema usisomeshe mtoto ili aje kukusaidia, hapana! Somesha mtoto ili akasaidie wengine. Hao wengine ndiyo watakuja kukusaidia wewe!
Hata hii ya kusema mchumba hasomeshwi ni kosa kubwa. We somesha huyo mchumba, ikitokea akakucha usijiue, badala yake mshukuru Mungu kwa sababu mchumba anasaidia mwingine.
Unajua kwa nini nasema hivi? Nasema hivi kwa sababu hata wewe hao wachumba wote uliowahi kuwa nao walisomeshwa na wengine.
Kwahiyo katika haya maisha usiache kutenda wema kila unapopata nafasi. Ukitenda wema kwa watu umejitendea wema mwenyewe. Wema wako ndo utafanya Mungu asikusahau!
Kwani hujawahi kuona kuna wakati anatokea mtu wakati wa shida zako, anakusaidia halafu anapotea? Yaani hata ukimpigia simu hapokei na meseji zako hajibu. Bila shaka hii imewahi kukutokea pia.
Hii ndiyo faida ya kutenda wema. Usiache kutenda mema kwa sababu eti unashida. Sikiliza! Huwezi kumaliza shida zako kwa kuwa mchoyo sana.
Tutatoa vingi kwa Nia ya kupata, lakini inawezekana tukapata kidogo au tusipate kabisa! Haha ndo maisha HUSIACHE KUTENDA MEMA! Utalipwa kwa majira yake!!!