Ma Producer hawa wamepotelea wapi..?

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,753
Mnamo miaka ya 2000 mziki wa Bongo fleva ulichangamka sana, pia ulichangamshwa kupitia wazalishaji wa muziki (producers) ambao walikuwa na vipaji pamoja na ushindani wa kweli,

kuna baadhi ya maproducer majina yao yalikuwa kutokana na ngoma walizo zalisha pia wasanii wadogo waliotengeneza majina kupitia wao kama Dullayo,

Hawa maproducer wako wapi

-Fundi Samweli
-J Rider
-Jay Eden
-Samtimba
-Kisaka (dawa yao)
-KGT
-Steve White
-Said Comorien
-Shirko
-Lil Ghetto wa Akhenato Record
-John B wa Grandmaster Record
-Dx wa Noiz Mekah
-Q the Don wa MO Record
-Kidbwoy wa Tetemesha Record
-Amba wa AB Music Room
-Allan Mapigo
-Bizman
-TC wa kama kawa record
-Dee Classic
-Duke


List ni ndefu naomba niishie hapo, enzi za muziki ulipoitwa muziki
 
Kidbwoy c ndo uyu wa mtandaoni anaejiita kidebway au ni tofauti ??


yes bishoo haswaaa
 
Kidbwoy c ndo uyu wa mtandaoni anaejiita kidebway au ni tofauti ??


yes bishoo haswaaa
hapana sio huyo, hapa tunamzungumzia KID BWOY Sandu George Mpanda zamani alikuwa mtangazaji wa RFA, Ndie aliewatoa kina Husen Machozi, Sajna, Baraka the Prince
 
Kwenye kazi ambayo unaweza kutrend ndani ya muda mfupi ni uprodyuza kwa hapa tz.

Watayarishaji ambao waliweza kukaa kwa takribani miaka kumi ni majani (p funk) na master j.

Wengi wa maprodyuza wakidumu sana ni miaka mitatu, mfano

2006- Mwaka wa KGT
2007-Marco chali
2008-Dunga
2009-Lamar
2010- bob junior
2011- Maneke
2012- Duke
2013 - shedy clever
2014 - Mone ganster wa clasic sound na nahreal
2015- Abi dadi
2016-2017-T touches
2018 to present - S2kizz

Kwa hiyo mkuu hayo mambo yako na msimu, kwa kifupi nilichokiona wengi wa watayarishaji hawako consistency.

Kuna mtindo wa wasanii kuhama hama studio, utakuta wakifululiza stdio moja basi wengi unawakuta huko.
 
Maproducer wameacha kuzalisha mziki wengi wao sababu mziki hauwalipi ,wamekuwa watu wazima amajukumu yanaongezeka malipo ni yale yale na wengi wao walioweka utaratibu wa malipo kila kazi yao itakapotumika wamekimbiwa.

Maproducer wa zamani wameacha mziki sio kwamba labda hawana content hamna,bali mziki hauwalipi na wasanii hawaheshimu creativity yao kwani wengi wao wanaamini bila wao,producer hawezi kuwa mkubwa mwisho wa siku Lamar kageukia katika Car wash yake na biashara yake ya chakula,Duke namuona anakampuni yake ya kutengeneza ferniture,kuweka partion kwenye maofisi ,Majani akawa yupo CMEA ,Master jay ana mishe zake nyingine,kwa kifupi kazi ya uproducer haina future nzuri.

Maproducer wa sasa hivi hata wakeshe studio lakini hawawezi kutoa product kama maproducer wa zamani .
 
DX Wa Noize Maker mbona yupo chaliangu asee!!Ananyonga midundo ya Jambo Squad na wahuni shazi apa Gachuland.
 
produyuza wangu wa muda wote
1.Lamar
2.p funk majani
3.KGT
4.Nahreel
5.C9
6.Duke tachez


dah hizo beat za Lamar aisee
 
Umesema vema mkuu ,zamani kweli biti zilikuwa nzuri hadi unafeel, kuna nyimbo zilikuwa zinatoka unaona msanii hakuna kitu ila biti inambeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…