HIBISCUS 80
JF-Expert Member
- Jun 18, 2020
- 1,058
- 1,218
Habari za kazi wanajamvi,
Leo hii nimeona niandike kuhusiana na umuhimu wa kuwepo kwa MAABARA za kufanyia majaribio mbalimbali katika Somo la sayansi kwa shule za msingi hapa nchini kwetu Tanzania.
Sayansi ni Somo ambalo mwanafunzi anatakiwa kujifunza kwa vitendo zaidi kuliko kwa maelezo (theory)
MAABARA ni chumba maalumu kimetengwa katika shule kwa ajili ya majaribio ya kisayansi.
Katika shule za secondari sayansi imegawanyika katika sehemu tatu nazo ni Physics, chemistry na Biology
Shule za msingi wanafunzi Wana Somo la sayansi ambalo ndani yake limebeba masomo hayo matatu yaani Physics,chemistry na Biology.
Katika shule za msingi hakuna kabisa MAABARA ili kuruhusu watoto wetu kufanya majaribio mbalimbali ya kisayansi.
Lakini kama kweli tunataka Kumjenga mtoto awe mahiri katika masomo haya basi majaribio hayo ya kisayansi yanatakiwa yaanzie shule za msingi .
Katika level ya shule ya msingi wanafunzi wanasoma topics mbalimbali ambazo zinahutaji majaribio badala ya kusoma kwa kumsikiliza mwalimu tu.Wanafunzi wanatakiwa kufanya zaidi wao wenyewe. kusoma kwa vitendo kunasaidia sana katika kumkuza mtoto katika mambo yafuatayo
1. CURIOSITY(UDADISI)
2. CREATIVITY(UBUNIFU)
3. CRITICAL THINKING
Kabla sijaelezea ni majaribio Gani wanafunzi wa shule za msingi wanapaswa kuyafanya katika masomo Yao ya sayansi ningependa kuelezea kwa kifupi kuhusu wanasayansi mashuhuri ambao waligundua mambo mbali mbali katika hii Dunia
Ukisoma historia za wanasayansi hao utagundua kuwa hakuna mwanasayansi ambae alilala usingizi akaamka na kugundua jambo Fulani
Au waliota ndoto ya ugunduzi , au walisoma kwa kumsikiliza tu mwalimu ndani ya chumba chenye pembe nne (darasa) na mara wakagundua jambo
Wanasayansi wote walitumia muda wao wote kujifunza kwa vitendo Tena kwa miaka kadhaa na kurudia experiments nyingi sana mpaka wakaweza kugundua mambo mbalimbali
Nitawataja wanasayansi kadhaa ambao walitumia muda wao mwingi kujifunza kwa vitendo na kwa kutumia idea za watu wengine waliotangulia wakaweza kugundua mambo mbalimbali
Archemedes - alitumia zaidi ya nusu ya miaka yake kujifunza na kufanya majaribio mbalimbali , ukisoma historia yake aligundua bouyancy force(upthrust), calculus, law of lever, odometer , pi (ambayo inatumika kutafuta area ya circles) nk
Galileo Galilei - aligundua simple pendulum, telescope,parabola, acceleration due to gravity nk, Galileo alitengeza telescope baada ya kujifunza kwa miaka mingi sana Tena kwa vitendo kuhusiana na lenses na hata alipotengeneza telescope alitumia kwa miezi kadhaa Kila siku kuangalia angani na akagundua kuwa Dunia na sayari nyingine zinalizunguka jua, hata alipofungwa kwa muda wa miaka Tisa aliendelea kufanya majaribio mbalimbali na kuchapisha maandiko yake
Sir Isaac Newton - universal law of gravitation and Newton"s laws of motion. Mchango wake umeleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa sayansi. Alitumia muda wake mwingi kujifunza nje ya darasa na kufanya majaribio mengi .historia inasema apple lilianguka juu ya kichwa chake ikapelekea UDADISI kwa nini apple lianguke chini na lisiende juu
Pythogoras - huyu alizaliwa ugiriki lakini alikwenda Misri na akaishi huko kwa miaka zaidi ya 20 kwa ajili ya kujifunza Alikuja na kanuni ya pythogoras
Wako wengine wengi kama Bohr,Robert Hooke, Rutherford, Dalton,Faraday ,Eistein nk. Wapo wanasayansi walioishi Miaka ya karibuni pia katika Karne ya 19 na 20 na wakagundua mambo mbalimbali, lakini hii yote inatokana na kujifunza zaidi nje ya darasa kwa kufanya majaribio mengi zaidi
Sasa nikirudi kwenye mada yangu hapo juu
Sayansi katika nchi yetu inafundishwa kama hadithi ya abunuwasi zaidi
Huwezi kusimamia darasani ukaanza kufundisha sayansi kama story au kwa kutumia picha za kuchora na picha za vitabuni
Hii inapelekea wanafunzi wengi kuona Somo hili kama SoMo gumu sana.
Jambo hili linatufanya pia kukosa wataalam wa kutosha katika sekta mbalimbali kama ujenzi, afya, maji, nk
Ndii maana utasikia watu wakisema hatuna ma engineer katika nchi yetu.
Kwa nchi za wenzetu watoto wadogo kabisa wa chekechea wanaanza kujifunza sayansi kulingana na level zao.
Kwa madarasa ya shule ya msingi Wana topics nyingi sana ambazo wanaweza kujifunza kwa vitendo na hata mazingira yanaruhusu
Walimu waache kuandika notes nyingiiiii badala yake wawape watoto nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kuwapa nafasi wanafunzi kutengeneza baadhi ya zana za kujifunzia badala ya kutumia manila Kila siku kuchora chora picha kwenye manila card
Mfano wa topics ambazo zitahitaji wanafunzi wa shule ya msingi kuingia MAABARA na kufanya majaribio na kutumia sayansi models kujifunza
Photosynthesis, archemedes principle, respiration,force,excretion, structure of leaves, digestion , reproduction in plants and animals,motion,acceleration,magnetism, electricity simple machines, ecosystem renewable energy,diffusion and osmosis,blood circulatory system,first aid,light energy,transfer of heat,temperature, aina za moto na jinsi ya kuzima, nervous system, types of food,acid and base nk
Hizo ni baadhi ya topics za shule ya msingi za sayansi katika shule zetu za Tanzania
Kwa kweli masomo ya sayansi hayana topic au sub topic ambayo mwalimu anatakiwa kueleza kwa mdomo
Kila topic na Kila sub topic inahitaji majaribio. Na hiyo ndio sayansi
Kuna models nyingi sana ambazo zinaweza kununuliwa na kuwekwa katika MAABARA hizo na wanafunzi wakaweza kutumia kujifunza kwa kuona
Pia baadhi ya topics wanafunzi wakatoka nje ya darasa na nje ya maabara na kujifunza kwani Kuna miti, mimea ,wadudu nk ambavyo viko nje wanafunzi wakajifunza.
Mwanafunzi anakimbia physics anasema physics ngumu halafu anaenda veta kusomea fundi umeme wakati anachokwenda kujifunza veta amekikimbia darasani
Lakini ni kwa sababu huko anakokwenda anajifunza kwa vitendo mwanzo mwisho
Lakini umeme anaojifunza veta unaanzia kwenye sayansi darasa la Tano na kuendelea ,pia anaukuta umeme Tena form two na form three na form four
Kujifunza sayansi ni gharama lakini hakuna jinsi ya kuepuka gharama hii kama tunataka kutengeneza wanasayansi mahiri
Kwa niaba ya Maarifa Time napenda kutumia picha zao nilizozikuta mtandaoni walitumia models kufundisha sayansi
Kuna model ya male reproductive system, Kuna model ya ecosystem nk
Models zingine hapo zimetengenezwa na walimu
Lakini sisemi walimu watengeneze models
Ila siku hizi models zinauzwa na zinapatikana
Kinachohitajika ni shule kununua na kuziweka maabara
Tuwafundishe watoto kuelewa na sio kukariri
Asanteni sana
Nawasilisha
Picha kwa hisani ya Maarifa- Time

Upvote
5