666999
Member
- Dec 25, 2018
- 29
- 31
Habari za wakati huu waungwana
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza uongozi na timu nzima ya Jamii forum kwa kutupatia tena nafasi ya kuandika juu ya mambo mbalimbali juu ya jamii yetu na taifa letu kwa ujumla.
Nikiwa kama mwana JF pia Mtanzania napenda kuchukua wasaa huu niandike kuhusu AFYA katika mambo matatu ya MAABARA,VIFAA VYA VYA KUJIFUNGULIA MAMA WAJAWAZITO NA HOMA YA INI
Kwa mujibu wa sera za serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya ni kwamba ifikapo mwaka 2025 kila kata iwe na kituo cha afya na kila kijiji kiwe na zahanati.
Pia kila mkoa uwe na hospital ya rufaa na kila Kanda iwe na hospital ya rufaa ya kanda
Kwa mwitikio huu tumeona hospital zote za mikoa zikipandishwa hadhi na kua hospital za rufaa za mikoa kwa kuboreshewa huduma kuanzia miundombinu,vifaa hadi watumishi na hii ili hospital hizo ziweze kupokea wagonjwa wa rufaa kutoka hospital za wilaya zilizo ndani ya mikoa husika,kwa hakika utaratibu huu umesaidia pakubwa kurahisisha huduma kwa maeneo husika na kuboresha afya za jamii husika
1. MAABARA
Kwa ngazi za kata na vijiji tumeona mwitikio ni mkubwa juu ya ujengwaji wa vituo vya afya na zahanati kwa kata na vijiji vingi hali iliyopelekea huduma za afya kufika karibu zaidi na jamii
Pamoja na uwepo wa hospital hizi asilimia 90 ya zahanati za serikali hazina maabara na zenye maabara hazitoi vipimo vya kutosha
Utakuta zahanati ina daktari mmoja na wauguzi kadhaa lakini haina fundi sanifu maabara (mtaalamu wa maabara) au haina maabara kabisa.
Vipimo utakavyoweza kukuta katika zahanati hizi ni kipimo cha haraka cha malaria (MRDT) na huduma za UKIMWI ambavyo pia hupimwa na watu ambao siyo wataalamu wa vipimo
Huku vipimo vingine vikiwa havipimwi kwa sababu ama hakuna maabara au hakuna mtaalamu
Pia kipimo kinapimwa na muuguzi au daktari ambae kimsingi kufanya kipimo siyo jukumu lake la msingi maana muuguzi na daktari siyo wataalamu wa maabara
Nashauri serikali kupitia wizara ya afya inapotuma watumishi katika zahanati mpya hasa za vijijini ihakikishe anaaajiriwa na fundi sanifu maabara/mtaalamu wa maabara walau mmoja kila zahanati
Uwepo wa mtaalamu wa maabara katika zahanati utamsaidia daktari kazi yake kua nyepesi na kutoa matibabu kua ya uhakika kwa sababu atatibu mgonjwa kwa uhakika kwa sababu ugonjwa utakua umetambulika baada ya vipimo kufanyika tofauti na sasa daktari anatibu kwa kuangalia dalili za mgonjwa
Mtazamo wangu kumtibu mgonjwa bila kupima badala yake unatumia dalili zake hii ni sawa na ramli tu kwa sababu magonjwa mengi yanafanana dalili
Faida ya wagonjwa kupimwa kwa ngazi ya zahanati utasaidia wahusika kutambua magonjwa yao mapema na kutumia dawa sahihi kabla ya ugonjwa kua mkubwa zaidi
Pia napendekeza serikali kupitia wizara ya afya iajili wataalamu wa afya wale walio Soma mwaka mmoja wa mafunzo waitwao LABORATORY ATTENDANT kwa ngazi ya zahanati kwa kua wanaajirika kwa urahisi na vipimo vinavyofanyika katika vituo hivyo siyo vingi na kufanya hivyo ajira zitakua zimewafikia kundi kubwa la watanzania
LABORATORY ATTENDANT wana uwezo mkubwa wa kuhudumia katika maabara zilizopo zahanati maana hata walioajiriwa katika hospital nyingi hapa nchini wanafanya vizuri
Kama Kundi la hawa LABORATORY ATTENDANT ni ngumu kuajiriwa na kufanya kazi bila kua na wasimamizi nashauri walau kila zahanati walau aajiliwe fundi sanifu maabara daraja la 3 (LABORATORY ASSISTANT)
Mwisho huduma za awali katika zahanati zikiboreshwa utakua msaada mkubwa kwa jamii na kupunguza mzigo mkubwa wa wagonjwa wengi kurundikana katika hospital za wilaya na hospital za rufaa za mikoa
2. VIFAA VYA KUJIFUNGULIA
Kitu kingine kwa umuhimu mkubwa vituo vingi vya afya vilivyoko vijijini vipelekewe vifaa vingi hasa vile vinavyotumika wakati wa kuzalisha wajawazito
Maana sera ya afya ya Tanzania kujifungua kwa mjamzito ni bure,lakini mjamzito wa nchi hii akienda kituo cha afya kujifungua zahanati huko kijijini lazima aende na vifaa vyake vya kujifungulia ndipo apatiwe huduma
Baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na mipira ya mikono na sindano
Jambo hili ni kero na usumbufu mkubwa kwa vituo vilivyoko vijijini
Hivyo nguvu kubwa ziwekwe kwa zahanati na vituo vya afya
3. HOMA YA INI(HEPATITIS)
Nashauri serikali kupitia wizara ya afya iweke nguvu kubwa kufikisha elimu ya ugonjwa wa Homa ya Ini kwa jamii kama ilivyo katika ugonjwa wa UKIMWI maana zaidi ya asilimia 80 ya watanzania hawana taarifa za kueleweka juu ya ugonjwa huu
Huku watanzania zaidi ya asilimia 95 wakiwa na uelewa na taarifa za kutosha juu ya ugonjwa wa UKIMWI
Kufanya hivyo taifa litakua na jamii yenye afya njema na ustawi mkubwa
Natanguliza shukrani.

Upvote
1