KYANYINIMARAIGA
Senior Member
- Oct 21, 2016
- 192
- 126
Kwanza kabisa nitanguize pongezi kwa Watanzania kwa kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru.Ni jambo la kujivunia kwa Watanzania ,kwani katika kipini hiki nchi yetu imekuwa na amani,ushirikiano na maendeleo ya kila aina.Mwenyezi Mungu tunakuomba uwape afya waasisi wa Taifa hili na uwarehemu wale waliotangulia mbele ya haki.Tunakuomba uwajalie uadilifu,weledi na afya viongozi na wanachi wote tuzidi kulinda uhuru wetu na amani.
Pili nawaomba wale wote waliobahatika kuuona utawala wa kikoloni na pia kushuhudia "Union Jack" ikishushwa tupeane salamu na pia maneno machache ya kukumbukwa katika matukio hayo mawili(utawala wa kikoloni na adha zake na siku ya uhuru na furaha zake).Hii ni kwa faida ya kizazi ambacho hakikubahatika kuona matukio hayo..