JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Leo ni siku ya kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani, ambayo inakwenda sambamba na maadhimisho ya haki za binadamu duniani kote.
Ukatili wa kijinsia ulikuwepo na umeendelea kuwepo katika jamii zetu licha ya kuwa wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakipaza sauti zao kupinga ukatili huo.
Ukatili huo umekuwa ukionekana kama mila na desturi kwa mtoto wa kike au vitendo hivyo kuonekana kama ushujaa kutendwa na watoto wa kiume bila kuangalia athari zinazopatikana kwa jinsia ya kike hivyo jamii kuvificha na kuvikumbatia.
Hivyo basi kila mwaka, tunaadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya kikatili kwa wanawake #16daysofactivism kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 ambayo ni siku ya kimataifa ya #HakiZaBinadamu
Hii ni katika kuashiria kuwa haki za wanawake ni haki za msingi za Binadamu na zinapaswa kuheshimiwa. Katika zama hizi ambazo mitandao imeshika hatamu, haki za wanawake mitandaoni zinapaswa kuendana na zile za nje ya mtandao.
Katika zama hizi za mitandao ya kijamii kumekuwakukifanyika ukatili kwa wanawake wa makusudi na kuleta athari kubwa na jamii ikifumba macho.
Je, ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni unaweza kuchukua sura ipi?
⁃ Kutumia au kusambaza picha za kingono za Mwanamke kwa lengo la kumdhalilisha.
⁃ Kufanya mzaha au kejeli kuhusu maumbile ya mwanamke.
⁃ Kumzushia uongo mwanamke ili kumsababishia kutoaminika au kuaibika kwenye jamii.
Pia nje ya mtandao au mazingira ya kijamii tunayoishi mwanamke au mtoto wa kike anakutana na mambo yafuatayo ambayo nayo ni ukatili dhidi yake.
-Vitendo hatarishi kwa mtoto wa kike vya ukeketaji au ndoa za utotoni, vinakatisha uhai na pia zinakatisha ndoto za mtoto na kudidimiza maendeleo kijamii. Hali hii pia huchochewa na wazazi kukumbatia wahalifu wakihofia kuharibu heshima ya familia.
Nini kifanyike kuzuia au kuondoa kabisa ukatili wa kijinsia?
Vitendo vya udhalilishaji au ukatili wa kijinsia havikubaliki kamwe katika jamii hivyo tunapaswa kuchukua hatua zenye mikakati dhabiti.
Miongoni kwa hatua za muhimu ni kuzuia ukatili huu kutokea kwa
-kuwapa elimu na uwezo watoto wetu wa kike kutoka katika umri mdogo ili wasiwe waathirika na kuwapa malezi watoto wetu wa kiume yanayowapelekea kuheshimu wanawake
-Wazazi pia wanapaswa kuwa makini na kutoruhusu wageni kulala chumba kimoja na watoto kwani ukatili mwingi hufanywa na ndugu wa karibu wa watoto tena maeneo ya nyumbani
-Muda wote watoto wakaguliwe kuhakikisha wako salama hasa mazingira wanayocheza na wenzao na kujuawanacheza nini na wanacheza na nani?
-Adhabu dhidi ya wanaofanya ukatili wa kijinsia ziongezwe ukali ili kujenga hofu na kupunguza matukio haya nchini hususani wanaume kuwabaka watoto au kuwanajisi watoto wa kike na kiume wenye umri mdogo na kuwasababishia maumivu, magonjwa na hata kifo
Kwa nguvu zote tupinge ukatili kwa kupaza sauti kwa pamoja kwa kila jambo linalotokea bila kuona aibu, kusita wala kuogopa. MWANAMKE NI JESHI KUBWA TUSIMAME PAMOJA kwa nguvu zote tupinge ukatili kwa kupaza sauti kwa kila jambo linalotokea bila kuona aibu

Upvote
0