Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani

Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Siku ya Afya ya Akili Duniani ni Siku ya Kimataifa maalumu kwa kutoa Elimu ya masuala ya Afya ya Akili, Uhamasishaji na Utetezi dhidi ya Unyanyapaa wa Kijamii pamoja na athari zake kwa wale walioathirika na Walezi wao

Shirika la Afya Duniani (WHO) linataja kuwa kabla ya janga la COVID19, takriban mtu 1 Kati ya 8 Duniani kote walikumbwa na matatizo ya kiakili, hata hivyo Msaada sahihi wa miundombinu na kiuchumi kwa ajili yao, ulikosekana

Matatizo ya afya ya akili yapo katika maisha yetu, familia, sehemu za kazi na jamii, na kuathiri kila mtu.

Dalili za matatizo ya akili ni pamoja na:

•Kuwa na hasira kupindukia
•Kukosa furaha katika maisha
•Kuwa na wasiwasi wa kupindukia
•Kukosa usingizi
•Kuwa na msongo mkali wa mawazo

Ni lazima tufanye kadiri tuwezavyo kuzuia magonjwa ya akili - kama watu binafsi na kama jamii

Ni muhimu kuendelea kutoa wito kwa serikali za kitaifa na za mitaa kuweka kipaumbele katika kupunguza mambo yanayojulikana kuwa hatari kwa afya ya akili ya watu Kama Ugumu wa Maisha, Migogoro ya Kijamii na Kimapenzi, Unyanyapaa wa Watu wenye Mahitaji Maalum pamoja na dhana au Mila potofu katika jamii

Pia kuimarisha wale wote wanashughulika na kulinda afya za akili kuanzia mtu Mmoja Mmoja hadi mashirika binafsi na kuunda nyenzo zinazohitajika kwa watu kustawi

Siku ya Afya ya Akili Duniani pia ni nafasi ya kuzungumza kuhusu afya ya akili kwa ujumla, jinsi tunavyohitaji kuitunza, na jinsi ilivyo muhimu kuzungumza kuhusu tunavyojisikia na kupata usaidizi ikiwa unatatizika

CHANZO: WHO, Mental Health Foundation
 
Maskini KATIBU hajaiona siku ya leo labda angepata hamasa asifikie kitanzi.
 
Oktoba 10 kila mwaka hufanyika maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), mtu mmoja katika kila kundi la watu nane huwa na changamoto ya afya ya akili huku sonona (Depression) ikitajwa kuwa kinara.

Changamoto za kila siku za maisha ya binadamu ndiyo chanzo kikuu cha matatizo ya afya ya akili. Aidha, uwepo wa majanga mapya ya kidunia hasa COVID-19 unatajwa kuongeza tatizo la afya ya akili kwa zaidi ya asilimia 25.

Pamoja na uwepo wa jitihada nyingi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kupambana na tatizo hili, ukosefu wa elimu ya kutosha kwa jamii, unyanyapaa na ubaguzi vinatoa changamoto kubwa katika kufikia malengo kusudiwa.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linatazamia uwepo wa dunia inayojali na kuthamini afya ya akili, usawa wa watu wote katika kufurahia haki zao pamoja na uwepo wa mifumo rafiki inayotoa upendeleo kwa kila mtu katika kupata msaada wa haraka anapokuwa na changamoto za afya ya akili.

Jikinge na changamoto za afya ya akili kwa kufanya mambo yafuatayo-
  • Husiana (Changamana) na wengine. Huongeza thamani yako na kufanya ujione ni sehemu ya familia yako, ukoo na jamii nzima kwa ujumla
  • Mazoezi huwa hayaishii kwenye kuongeza utimamu wa mwili pekee bali huchangia mienendo chanya ya mihemko ya mwili. Shiriki mazoezi.
  • Kuwa na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Pia jifunze kuchukua likizo fupi pindi unapohisi kuwa baadhi ya mambo unayoona huko yamekuwa chanzo katika kukukosesha furaha.
  • Usiwe mgumu kuonesha hisia zako kwenye nyakati zote za maisha pasipo kujali jinsia yako. Penye changamoto vunja ukimya, eleza yanayokusibu.
  • Kuwa mkarimu. Aidha, tabia njema za kushukuru, kusamehe, kuomba msamaha wengine pamoja na kuridhika na mafanikio binafsi pasipo kujilinganisha na wengine husaidia kuilinda afya ya akili.
  • Jiepushe na matumizi ya dawa za kulevya
Chanzo: WHO / Mental Health Tanzania
 
Back
Top Bottom