Maadui sita(6) hatari katika maisha yako.

Maadui sita(6) hatari katika maisha yako.

Alvin_255

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2015
Posts
246
Reaction score
503
Kwenye maisha unayoishi huwezi kuepuka maadui ambao wanakuchukia, wasiopenda kukuona umefanikiwa bila kujali upo sehemu gani na unafanya nini,

Joel Nanauka kawaongelea "Maadui 4 hatari katika maisha yako" ambao ni Kaini, Delila, Penina, na Hamani. (Una mengi ya kujifunza kupitia JN).

Kwa lengo la kujifunza zaidi kuna wengine maadui wawili ambao wanafikisha idadi ya maadui 6 hatari sana waliojitokeza katika MAANDIKO MATAKATIFU unaopaswa kuwa makini nao ambao ni Adui mkewe Potifa na Adui Kora...

Maadui hao 6 katika maisha yako Ni hawa:-

1. Adui Kaini.(Kaka yake Habili)

Aina hii ya mtu anaweza kuwa ni. Ndugu, rafiki au mtu wako wa karibu zaidi katika maisha yako kama alivyokuwa Kaini kwa Habili, wakati mwingine huwezi kufikiri kama anaweza kuwa ni adui yako kwa ukaribu mlionao, kazi zake yake kubwa ni hapendi mafanikio yako atakuonea wivu pindi anapoona mafanikio yako Aina hii ya adui atakufanyia ubaya katika maisha yako bila wewe kujua, atakufanyia ubaya Kisha atajificha ili asionekane kuwa ni mbaya kwako. Kuna wakati unaweza pitia magumu yeye atajionyesha Kama mfaraji wako lakini kumbe ndoo mhusika wa magumu unayopitia, utacheka nae vizuri, utakula nae lakini atayaonea wivu mafanikio yako wakati mwingine unaweza kuwa msaada kwake lakini mwisho wa siku atakusaliti, atakuumiza au atakuangamiza kabisa . Na hichi ndicho kilichomtokea Habili. Ni muhimu Sana kumuomba MUNGU ili umjue adui Kaini katika maisha yako.

2. Adui Mkewe Potifa.

Ni aina ya adui katika maisha yako ambaye atajitokeza kwako kwa tamaa zake za mwili ili akuharibie hatima ya maisha yako. Aina hii ya adui tamaa za mwili wake zitavutiwa na mwonekano wako, uzuri wako, elimu yako, kazi yako, kipaji chako, karama yako ili afanye na wewe uzinzi au uasherati. Aina hii ni miongoni mwa adui wanaoharibu hatima ya maisha ya watu wengi Sana, Ikiwa utajirahisha kwake atakupata na utafanya nae uzinzi au uasherati lakini matokeo yake ni majuto yenye maumivu ya machozi yatakayoacha alama katika maisha yako. Kupitia Aina hii ya adui wengi wamepoteza ndoto za maisha yao, wamepoteza mahusiano yao kwa watu waliokuwa wakiwaamini, wameharibu ndoa zao, wameharibu afya za miili yao. Ikiwa Yusufu alimshinda adui huyu hata wewe unaweza mshinda pia kupitia kauli hii " Nifanye ubaya huu mkubwa nimkosee MUNGU?"

3. Adui Kora..

Ni aina ya adui hatari katika maisha yako atakayekupinga katika kila kitu, hataufanye mazuri kiasi gani yeye anona mabaya tuu. Kama wewe ni kiongozi Aina hii ya adui atawashawishi hata baadhi ya watu unaowaongoza wajumuike nae katika kupinga uongozi wako, ataonyesha ukosoaji katika kila unachokifanya hata kama ni kizuri, atakuchukia bila sabababu yoyote ile.Aina hii ya adui unapaswa kumuomba MUNGU sana amuaibishe katika maisha yake, usipigane nae wala kubishana nae muombe MUNGU akushindie vita hii, Kama ilivyomtokea Kora dhidi ya mtumishi wa MUNGU Musa katika safari ya wana wa Israel..

4. Adui Delila...

Ni adui anayechunguza taatifa za maisha yako, kazi yake kubwa ni kukupeleleza au kuchunguza zaidi kuhusu siri za maisha yako, aina hii ya adui atachunguza au kupeleleza siri za maisha yako , atataka kujua kila kitu kinachokuhusu wewe, Aina hii ya mtu akija kwenye maisha yako ataishi na wewe Hadi kwenye kiwango utakachomwamini zaidi, lakini ataitumia hiyo nafasi kwa ajili ya kupata taarifa za maisha yako azipeleke sehemu fulani ikiwa zitahitajika ili akuangamize. Hichi ndicho kilichomtokea Samsoni, Delilah alimpeleleza siri ya nguvu zake na akaipeleka Siri hiyo kwa walio mtuma hali iliyopelekea maangamizi ya Samsoni. Katika maisha tunayoishi aina hii ya adui inazidi kuharibu mahusiano ya watu, familia za watu, kazi za watu, biashara za watu. Muombe MUNGU akusaidie kumjua na akushindie vita hii ya adui huyu hatari wa maisha yako, peke yako huwezi...

5. Adui Penina.

Penina ni mwanamke aliyemnyanyasa sana Hana katika wakati ambao hajapata mtoto,aina hii ya mtu katika maisha yako, kazi yake kubwa ni kutangaza madhaifu yako pia kukukejeli, kukudharau na kukuchekea kupitia magumu unayopitia katika maisha yako.Aina hii ya mtu katika maisha yako atakuchukia na hapendi kuona mafanikio yako, atacheka na kufurahi zaidi anapokuona una pitia mambo magumu katika maisha yako. Aina hii ya maadui tunaishi nao sana katika maisha yetu hapa duniani furaha yao nikutuona tunazidi kupiti magumu katika maisha yetu, Zidi kumwomba MUNGU zaidi ili wanaokucheka na kukuwazia mabaya MUNGU awaabishe kupitia mafanikio yako.

6.Adui Hamani.

Adui hamani ni adui hatari Sana katika maisha yako yuko tayari kukuona unakufa au anakuondoa yeye mwenyewe duniani kwa kukuua kwa chuki aliyonayo kwako. Aina hii ya adui kazi yake kubwa ni kukuona umekufa kaibasa katika maisha haya, kwa wale ambao mmesoma kisa chake Hamani alimchukia Mordekai ambaye alikuwa ni mlinzi tuu wa getini wakati yeye ni Kiongozi mkubwa zaidi wa mfalme, Aina hii ya adui anaweza kuwa amekuzidi kila kitu katika maisha yako lakini bado akakuchukia wewe, mafanikio yake makubwa ni amekupoteza KATIKA maisha haya, yuko tayari Kutoa hata pesa ili akuharibie mahusiano, ukaharibe kazi yako, ukaharibie biashara yako na wakati mwingine yuko tayari kukuona umekufa kabisa katika dunia hii.Muombe MUNGU sana ili akushindie vita hii ya adui huyu Hamani, peke yako huwezi.

MWISHO....

Muombe MUNGU akusaidie kuwajua adui zako katika maisha yako, na ushinde kila vita ya adui wanaojitokeza katika maisha yako.

Ombi lako wakati wote liwe ni...

"Ee MUNGU, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu.". ( Zaburi 51:1)



"Afya yako ya Akili, Kipaumbele chetu"
 
Back
Top Bottom