Mara baada ya kupata uhuru baba wa taifa hayati Mwl. JK Nyerere aliainisha na kutangaza maadui wakubwa wa taifa letu. Mwl. JK Nyerere alitangaza maadui wa taifa kuwa ni maradhi, umaskini na ujinga. Tangu kutangazwa kwa maadui hawa wa taifa, taifa liliwapinga kwa nguvu zote na kusaidia kuwatokomeza kwa asilimia kubwa ambapo kwa sasa ujinga sio tishio kwa taifa tena umasikini japo bado upo lakini sio kama kipindi kile tunapata uhuru, lakini pia maradhi yanadhibitiwa kwa uboreshaji mkubwa wa huduma za afya.
Kwa manufaa ya Tanzania tuitakayo ni lazima tukae chini na kuweza kuwatangaza maadui wa uchumi wa taifa letu na kuweka mikakati juu yake na kupigana nao kama taifa kama ilivyokuwa kipindi cha baba wa taifa. Taifa kwa sasa tuna maadui ambao kwa ujumla ni tishio kwa usalama wa uchumi na ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ya Tanzania.
Ufisadi ni adui namba moja kwa ukuaji wa taifa letu, tena inawezekana tupo katika halii duni ya uchumi ni kwasababu huyu adui ndo analitafuna taifa kwa asilimia kubwa. Pesa za miradi zinatoka lakini miradi haikamiliki au inakamilika chini ya kiwango na pesa zingine zinaishia kwenye mifuko ya watu wachache wasio na uchungu na maendeleo ya taifa lao. Katika swala la mapato waliopewa dhamana ya kukusanya badala ya kuweka pesa itumike kwa maslahi ya taifa wanajibinafsisha kwa matumizi yasiyofaa na hivyo kufanya makusanyo kuwa madogo kwenye hazina ya Tanzania tuitakayo ni Tanzania yenye usawa na maendeleo sasa tunaweza kuongeza Kodi kwa wafanyabiashara, tukatoza tozo za Kila rangi na vyanzo vingine vya mapato lakini hatuwezi kufanya chochote kwakuwa ufisadi ni hatari sana kwa fedha zinazopatikana serikalini na hata kwa mali za serikali pia, ni lazima ufisadi ushugulikiwe kama adui namba moja wa taifa letu ili kuijenga Tanzania bora ya miaka kumi ijayo.
Rushwa ni adui mkubwa wa haki na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla, rushwa ni moja ya vitu ambavyo huinua ubaguzi ndani ya nchi kwa matabaka ya pesa na wasio navyo, huzalisha uvunjifu wa sheria na ukanyagaji wa katiba ya nchi na kiuhalisia inaweza kuficha uovu mwingine na kushindwa kuwajibishwa kwa aina fulani ya kundi la watu kwenye utendaji. Rushwa lazima atangazwe kama moja ya maadui wakubwa wa taifa letu kwa ujenzi wa Tanzania bora tuitarajiayo, utekelezaji wa adhabu kwa wahusika iwe ya ukali ili kudhibiti, katika Tanzania yetu rushwa imeota mizizi inahitaji miaka mitano mpaka 10 ya kushugulika na huyu adui kwa ukamilifu kabisa ili usawa na haki zitendeke katika jamii na uwajibikaji uwe wa hali ya juu. Mataifa yote yaliyoendelea duniani rushwa kwao ni kwa kiwango kidogo sana, hivyo kama tunahitaji taifa lisilo kandamizi, lenye uhuru, haki na usawa kwa watu wote rushwa lazima ipingwe kwa nguvu zote.
Spirit (Vilevi vikali) na energy drink, ni vinywaji ambavyo kwakweli vinaliingizia taifa Pato kubwa kwa kuwa kodi inalipwa katika nchi yetu kupitia uzalishaji mpaka kwa mtumiaji wake lakini ni vinywaji ambavyo ni hatari kubwa sana kwa vijana wa taifa letu vilevi vikali(spirit) huathiri kwa ukubwa ufanisi wa kazi kwa vijana na wengi kuwafanya kuwa tegemezi. Energy drinks huwapa vijana nguvu kubwa na hamasa ya kufanya kazi iwapo itatumiwa vizuri lakini Ina madhara makubwa sana kwa mtumiaji endapo itatumiwa kihilela na kwetu hapa inatumiwa holela na hivyo kuwa mwiba kwa vijana ambao ni rasilimali ya taifa. Vinywaji hivi viwekewe mazingira ya kutumika ipasavyo kutumika ili kupunguza madhara na kuwafanya vijana wajikite katika kufanya kazi sana na sio kutumia muda mrefu katika ulevi ambao huwafanya tegemezi bila kuwa na dira. Taifa la sasa linaonekana kuwa na vijana wengi wa hovyo ni kwasababu ya matumizi ya hivi video.Hivyo ili kujenga nchi bora vijana lazima wawekewe mipaka katika matumizi ya vileo hivi.
Kamali (Michezo ya kubahatisha) imekuwa ni kitu cha kawaida sana katika jamii yetu hasa kwa vijana kushiriki katika Michezo ya kubahatisha ovyo ovyo, mashine za kuchezeshea kamali zipo kila sehemu na hizi zinaharibu akili na mitazamo ya vijana wengi kutoka kuamini katika kufanya kazi kuja kuamini katika bahati nasibu, Michezo ya kubahatisha iwekewe mikakati maalumu iwe na sehemu maalumu na wakati maalumu na sio inazagaa mitaani mpaka kwa mangi hii ni hatari sana kwa kizazi hiki cha taifa hili. Vijana wengi wanashinda asubuhi mpaka jioni sehemu za kuchezea kamali na kuwafanya wasiende hata kwenye utafutaji wa Kila siku na wengi kuishia kuwa wavivu. Hatuwezi kuijenga Tanzania ilibora na vijana ambao wanashinda wakisubili kubahatisha maisha, ni lazima tufundishe vijana wetu kuyatengeneza maisha na sio kusubili kubahatisha.
Hivyo kama taifa lazima tuainishe maadui wakubwa wale ambao waliathiri kundi kubwa la watu na kushughulika nao kwa upana na makini ili kuokoa kundi hilo na kuijenga nchi bora tuitakayo.

Upvote
3