Maafa Mnacho secondari, Ruangwa-Lindi

southern

Member
Joined
Feb 10, 2012
Posts
25
Reaction score
0
Wadau, habari zenu hapa jamvini....

mnamo tarehe 03 feb 2012, majira ya saa 10 jioni, shule ya sekondari mnacho iliyoko wilayani Ruangwa mkoani Lindi ilikumbwa na balaa la kimbuga lililoendana sambamba na mvua kubwa hivyo kusababisha kuezuliwa kwa mapaa ya madarasa, ofisi ya mkuu wa shule, ofisi ya waalimu na nyumba moja ya mwalimu.

kutokana na balaa hili, wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakisoma kwa shifti wakitumia madarasa matatu yaliyobaki...



naomba kuwasilisha...
 
poleni sana wana mnacho, naamini mamlaka husika (wizara, wilaya na mkoa) zitashughulikia swala hili mapema illi kurudisha utulivu na ratiba ya shule irejee kama kawaida.
 
Poleni wakazi wa mnacho pande za kwetu
 
Kamati ya maafa ya Wilaya na Mkoa inapaswa kuliona hilo! Je, ngazi ya wilaya na mkoa wanazo hizo taarifa za maafa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…