Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Nimepita sokoni hapo jana, nimekuta akina mama wamepanga mboga zao chini wakiwa wametandika mfuko lakini nyingine zipo karibu na matope na nyingine zinarushiwa uchafu zikiwa hapohapo.
Maafisa Afya wapo, wanafanya nini sijui! Ni muhimu kuchukua hatua za haraka kurekebisha hali hii, ikiwezekana wanaoweka bidhaa chini wawe na utaratibu wa kuwekewa meza ili kuwa mbali na matope na uchafu uliopo kwenye ardhi.