kwa sasahivi utaratibu wa ajira serikalini Tanzania bara katika wizara zote, mikoa yote, halmashauri zote za wilaya, miji na majiji lazima zinaratibiwa (kutangaza na kuajiri kwa niaba ya hizo ofisi) na sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma ambao wao ndio wanatangaza kwenye vyombo vya habari na mara nyingi naona hata huku jamii forum watu wenye nia njema wanapost hayo matangazo ya ajira za serikali ili watu wenye sifa waziombe. wao ndio wanatangaza, wanashortlist na kufanya usaili. huyo kigogo unayemtaja wa huko simiwi nadhani atakuwa tapeli achana naye. Nakushauri usubiri zikitangazwa ndipo uombe kwa wahusika jinsi tangazo litakavyotoka