Maafisa mikopo: Vituko na vimbwanga vya wateja!

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Kwa ambao tumewahi au tunafanya kazi hii, kwakweli ni kazi yenye changamoto sana hasa kwenye taasisi hizi ndogo ndogo (Microfinance). Mara nyingi wateja wetu huwa ni wasumbufu na wakati mwingine hufanya vituko kiasi kwamba ukimuelezea mtu anaweza asiamini!
Ni jambo la kawaida kabisa mteja kuhama nyumba anayoishi usiku ili kukimbia kulipa marejesho. Wengine wanaanzisha utaratibu wa kuondoka alfajiri na kurudi usiku mwingi. Baadhi ya wateja pia huwa wakali sana au kujificha pale wanapowaona maafisa na wengine hufikia hadi kutoa sime, mapanga na silaha nyingine kuzuia mali zao walizoweka kama dhamana zisichukuliwe. Kama uko katika sekta hii karibu tushee vituko vya wateja wetu.
 
Wengine wanakwambia wanauguza wana wagonjwa anakwambia hospitali ya mbali ambayo sio rahisi ufike. au anakwambia amelazwa Morogoro au anakwambia yuko kwenye msiba mkoa mwingine. Kiboko yao anakwambia wala hunidai ili umpeleke mahakamani alipe kidogo kidogo.
 
Mjue kutunza siri za wateja wenu huko makazini kwenu, ungekuwa Daktari wagonjwa si wangekomaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…