Maafisa ugani wanatatua matatizo kwa usahihi?

hauleibrahim

Senior Member
Joined
May 17, 2024
Posts
183
Reaction score
125
Poleni sana wakulima wa Tanzania na michaka michaka ya kilimo na kupambana kujitafuta chakula Cha familia na pesa za kumaliza matatizo ya siku.

Kwa hawa Maafisa Ugani tunaoambiwa huwa wanapewa pikipiki za umma kuja kupitia mashambani kwa umma Kwa wakulima hivi huwa mnafanya nao kazi vipi na wanatatuaga matatizo Kwa kiwango sahihi.

Kama umewahi kuwaita maafisa ugani je ulipata ufumbuzi sahihi wa kinacho kusibu shambani mwako iwe magonjwa au ubora finyu wa mbegu n.k

Swali langu hawa maafisa ugani Kwa kila baada ya mwaka wa kilimo hivi wanairipoti zozote wanazo andika na kuziwakilisha kwenye mkoa kuendana na tafiti za kero za mkulima alizo waitia mashambani ili zifanyiwe ufumbuzi msimu mwingine wakulima wasikwame na changamoto zilizopita.
 
Tueleze kwanza umekutana na mkasa Gani?
Sijakutana na mkasa ila Niko kupata abc kuhusu hawa watu deep Kuna vitu nataka niwatafutie nifanye andiko lisilo na ufinyu wa mawazo juu ya utendaji kazi wao Kwa mkulima wa chini anae taka kuwa tajiri nchini
 
kutokana na maelezo yako yakubidi kukutana na wakulima ili andiko lako liwe na uhalisia.
 
Kiufupi mm ni mkulima nae uliza hiki na nipo hku shambani njombe makambako je hpo UNa maoni mengine
 
Kama ni mkulima basi una majibu ya kutosha kuhusiana na huduma za ugani eneo lako hilo. Utafiti wako utakuwa na mashiko kama utakutana na wakulima moja kwa moja ila huku mtandaoni ni vigumu Sana.
 
Sampling frame yako inabidi uchague mkoa hususani mkoa unaoishi, Kisha chagua wilaya kadhaa, katika wilaya hizo chagua vijiji kadhaa na katika vijiji hivyo chagua idadi ya wakulima wa kufanya nao kazi kwenye utafiti wako. Baada ya hapo changanua takwimu zako Kisha Njoo na andiko.
 
Majibu sina ndo mana nimefanya andiko hilo Kwa wazoefu wanipe majibu ambayo yatanipa pa kuanzia nikitakacho ndani y sekta ya kilimo.
Kama ni mkulima basi una majibu ya kutosha kuhusiana na huduma za ugani eneo lako hilo. Utafiti wako utakuwa na mashiko kama utakutana na wakulima moja kwa moja ila huku mtandaoni ni vigumu Sana.ningekuwa na
 
Poleni sana wakulima wa Tanzania na michaka michaka ya kilimo na kupambana kujitafuta chakula Cha familia na pesa za kumaliza matatizo ya siku.

Kwa hawa Maafisa Ugani tunaoambiwa huwa wanapewa pikipiki za umma kuja kupitia mashambani kwa umma Kwa wakulima hivi huwa mnafanya nao kazi vipi na wanatatuaga matatizo Kwa kiwango sahihi.

Kama umewahi kuwaita maafisa ugani je ulipata ufumbuzi sahihi wa kinacho kusibu shambani mwako iwe magonjwa au ubora finyu wa mbegu n.k

Swali langu hawa maafisa ugani Kwa kila baada ya mwaka wa kilimo hivi wanairipoti zozote wanazo andika na kuziwakilisha kwenye mkoa kuendana na tafiti za kero za mkulima alizo waitia mashambani ili zifanyiwe ufumbuzi msimu mwingine wakulima wasikwame na changamoto zilizopita.
Hawa maafisa ugani huandika Taarifa ya kila mwezi(Monthly Report) na kuiwasilisha Ofisini ngazi ya Wilaya (Ofisi ya DALFO/DED). Wilaya huziunganisha Taarifa hizo na nyinginezo za Sekta mbalimbali na kuzituma Mkoani.
Wewe kama unafanya Utafiti wa Mazao au Mifugo ni vyema ukaenda kwanza Ofisi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kujitambulisha na kupata Baseline data na Ushauri wa namna ya kuendelea na Utafiti wako. Aidha Ofisi inaweza pia ikakupa msaada kwa kukupa mtaalam wa fani husika atakaye kupa company au kukuongoza ili upate kile unachohitaji. Kinyume na hapo eti ww binafsi ukajiingilia mashambani au kwa wafugaji (mifugo au samaki) na kuanza kudodosa wakulima bila kuwa na mwenyeji wako unaweza kukosa unachotaka na wakati mwingine wakulima wa Mazao au Mifugo wakakukataa na ukishupalia maswali yako ukapata mkong'oto. Siku hizi wakulima wapo macho sana na Utapeli au Shughuli zisizo Rasmi ndani ya maeneo yao.
Mtiririko utakaoifanya shughuli yako iwe ni shughuli Rasmi na Halali ni wewe kupita kwa DED, Idara husika, Ofisi ya Kata then ndo uende kijiji unacholenga au kinachokidhi kwa mujibu wa sample design yako.
Maafisa hao ukiwaita wanafika (labda kuwe na kikwazo mahali) lakini pia usisahau matokeo katika kile wanachofanya au Ushauri wanaotoa sio ya papo kwa hapo. Inachukua muda kuona matokeo ama ni mazuri au ni mabaya. e.g. kama ni ugonjwa wa mifugo (ng'ombe, mbuzi au kuku) matokeo ya Tiba ni baada ya siku 3-5 au hata mpaka siku 15. Kwa upande wa mazao, kama ni ukosefu wa rutuba e.g. Nutritional deficiency , ukiweka mbolea matokeo ni baada ya wiki 1-3 au hata zaidi kutegemea na aina ya mbolea uliyotumia (Natural au Industrial)
 
Acha ubishi hapa huwezi kupata unachotaka.
Kwa nn siwezi kupata nipe sababu nisizo weza kupata usiseme siwezi bila sababu humu Kuna watu mtambuka.

Ñipe sababu usiseme siwezi tu bila kunipa sababu za kutokuweza
 
Umejibu vzuri

Umejibu vizuri nimekuelewa japo natamani kuuliza swali.ww ni mkulima ama mfugaji mana umetoa maelezo ila sijui una idea tu ya maelezo au we umewahi nufaika na hiyo process kama ndio Nina maswali kwako kadhaa.
 
Ufanyaji kazi wao unategemea na muitikio wa wakulima namna wanavyomtumia hasa afisa ugani (kilimo) awezi washa pikipiki anaenda tu lazima awe na mihadi na wakulima eneo husika coz Awana posho za mafuta licha ya kuwa na usafiri.

Pili wanapokea maelekezo kudili na mazao au kufatilia wakulima flani wakishirikiana na watendaji wa vijiji mfano mzuri Hawa wataalamu wapo wachache sana hasa hizo wilaya za mkoa wa njombe kila kata yupo afisa mmoja na ukubwa wa kata nafikili unaujua vizuri.

Pia mazao mengi ya kibiashara unakuta makampuni yanayowekeza Yana mabwana shamba wao parachichi, chai, pareto , kahawa n.k

Hivyo afisa ugani wa serikali awezi kuweka nguvu kubwa ya kushawishi isipokuwa kukusanya tu takwimu na kero ndogo ndogo na kuziwakilisha eneo husika kama Kwa mkuu wa idara na wakati ikitokea changamoto kubwa ndipo uandaa mkutano kutoa mafunzo Kwa wakulima kama uvamizi wa viwavi n.k
 
Kwa nn siwezi kupata nipe sababu nisizo weza kupata usiseme siwezi bila sababu humu Kuna watu mtambuka.

Ñipe sababu usiseme siwezi tu bila kunipa sababu za kutokuweza
Nimekushauri nenda field uka wa face wakulima ana kwa ana ukiwa na questionnaire yako. Toka juzi umeanzisha thread lakini mpaka Leo umepata wachangiaji wangapi? Unafikiri kwa nini wachangiaji ni wachache?
 
Umejibu vzuri

Umejibu vizuri nimekuelewa japo natamani kuuliza swali.ww ni mkulima ama mfugaji mana umetoa maelezo ila sijui una idea tu ya maelezo au we umewahi nufaika na hiyo process kama ndio Nina maswali kwako kadhaa.
Uwe na amani. Uliza tu mkuu, nitajitahidi kujibu kadri niwezavyo. Ur most welcome. Huku kuna shida ya umeme; kwa hiyo ukiona nimechukua muda kutoa jibu pengine ni kutokana na hiyo changamoto. Natumia PC.
 
Back
Top Bottom