A
Anonymous
Guest
Habari Wana JF, binafsi nipongeze Jukwaa hili la Fichua Uovu, nimekuwa naliona mara nyingi sikuwa najua jinsi ya kulitumia, nimepata msaada kutoka kwa memba mwenzangu, nami nimeona nilitumie inavyotakiwa kutoa dukuduku langu.
Sisi vijana wadogo ambao tumeamua kujiajiri kwa kupambana tunateseka na kibaya zaidi wanaosababisha tuteseke ni watu wachache ambao wanatumia nafasi zao za madaraka kwenye mamlaka vibaya.
Mimi niko Arusha, Wilaya ya Arumeru, Kijiji cha Tengeru ni mfanyabiashara mdogo, nina chumba cha biashara Tengeru, mimi na wenzangu tunapitia mateso makubwa kutoka kwa Halmashauri na mmoja kati ya anayetesa vijana anajulikana kwa jina maafuru la LUKUMAY.
Kila mwezi tunalipa shilingi 60,000 kwao, hapo bado tunatakiwa kulipa kodi ya pango lakini kinachotoa hasira zaidi LUKUMAY na wenzake wanaweza kuja zaidi ya mara tano kutaka uwape hela.
Kibaya zaidi wanatupa vitisho kuwa hakuna kitu tunaweza kufanya kuzuia hicho wanachokifanya, kuna siku akatamka “Nikiamua kukutesa nakutesa has ana huna cha kunifanya.”
Watanzania tunaishi katika Nchi yet uhuru ila mateso ni mengi, mtu anakwambia waziwazi kuwa naweza kufanya chochote hii biashara yako na usinifanye chochote, kweli maisha ya hovyo sana haya.
Naingiza kipato kidogo lakini natoa kingi kwenda Serikalini, ipo siku vijana tutachoka, Serikali yetu itusaidie watu kama hawa ndio chanzo cha kufanya tutengeneze chuki dhidi ya viongozi na Serikali yetu.