Maafisa wa itifaki na wa usalama wako wapi?

Maafisa wa itifaki na wa usalama wako wapi?

babykailama

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
251
Reaction score
243
MAAFISA WA ITIFAKI NA WA USALAMA WAKO WAPI?:thinking:


Bila ya kujali ukweli wa kilichotokea, bado naona kuna kitu hakijakaa sawa juu ya namna Naibu Waziri Malima alivyoonana na Waandishi wa habari na zaidi ya yote pia majibu yake juu ya alivyoibiwa na alichokuwa nacho.

1. Imekuwa mapema sana, je, ni kwa nini Mwakilishi wake (Afisa wa Itifaki) asingeonana na Wandishi na kueleza kwa kifupi sana kama ifuatavyo:

Tunakiri kwamba leo Naibu Waziri ameibiwa mali kadhaa akiwa hapa Hotelini. Kwa sasa yeye na vyombo vya Usalama wanawasilisha taarifa kamili juu ya wizi uliotokea huko Polisi. Uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na Viongozi wa Hotel ambao nao wamekiri kuwepo kwa uvunjaji sehemu ya mlango. Idadi kamili ya kilichoibiwa na maendeleo ya uchunguzi wa wizi huu mtajulishwa rasmi na vyombo vya Usalama husika wakati ukifika.

(Hakuna cha kupokea swali lolote, kisha anaondoka kwa kusema)

Kumradhi, sitapokea swali lolote wala kujibu lolote kwa sasa maana suala liko mikononi mwa vyombo husika.


2. Je kuna ulazima gani Waziri kuanza kueleza kuwa ana bastora na bunduki? Huko ni kujiexpose zaidi kuliko anavyodhani kuwa anaonyesha kuwa na usalama madhubuti. Aidha yeye kutoa maelezo yanayoonyesha kuwa Viongozi wetu wanasafiri kwa KUJIHAMI wao wenyewe dhidi ya ‘wabaya’ ni kuonyesha kuwa kuna udhaifu mkubwa sana katika mfumo wetu nadani ya wana Usalama wa Taifa, Wapambe wa viongozi na hata Askari Polisi maana popote alipo wote hao huwa wapo tena wakiwa full equiped! Hana haja ya kujisema kuwa anajilinda hata kama ni kawaida.

3. Je kuna ulazima gani Waziri kuanza kutoa maelezo yanayoweza kuibua maswali kibao juu ya jinsi mfumo na matumizi ya fedha za Serikali unavyofanya kazi,eti “natembea na vijisenti “( kiashiria cha dharau kwa fedha nyingi machoni pa mlipa kodi ambazo pia ni malipo halali ya Tanzania) kwa maelezo finyu eti anakuwa amejiandaa maana Bosi wake akishindwa kwenda sehemu yeye inabidi amwakilishe! Hivi kweli kazi ya kubeba hizo fedha zote ni yake Naibu Waziri? na je ni lazima Kiongozi wa juu kama yeye abebe fedha nyingi hivyo hata leo katika karne ya M-; Tigo-; Airtel-; Voda – Pesa, ATM Kibao kila Manispaa na zaidi ya yote kuaminika kwa Taasisi ya Uwaziri katika watoa huduma woyote nchini kama kuna dharura yeyote imeibuka! Na hata safari ikiibuka, je ni yeye mwenyewe inabidi ajitafutie ticket ya ndege na bookings za hotel au anabukiwa na mtu fulani wa Itifaki husika? Kama ndivyo, basi huyo ndiye angekuwa mhanga wa wizi huo na si Naibu Waziri! Nisemacho ni kuwa Naibu Waziri angekutwa na fedha kiasi kidogo tu cha matumizi yake.

Hivi hakuna watu wa Itifaki wala wana - Usalama ambao wanatakiwa kuwa wanatoa ushauri wa nguvu na hata ikibidi kutoa onyo kwa Viongozi wasiwe wanatoa matamko ambayo yanaweza kuidharirisha Serikali yetu na hata kwa wakati mwingine kuwaingiza katika matatizo zaidi?

Mniite kwenye semina elekezi!!
 
Hii nafikiri MH alikua anajisafisha. kwa akili yangu ndogo nahisi Mh alikua na totoz ambayo ilimtoka na ikamlazimisha kuto kuzingatia itifaki na kuamua ku clear mambo kabla wadaku hawajainasa.
 
hii habari ilivuja kwa kasi ya ajabu bila yeye kutegemea,, na story ilisambaa kua ameibiwa na changu.., nadhani wanaomfahamu walimjulisha kuwa mambo yapo hadharani,,

sasa kwa kupanic na bila kujipanga ndo akaita waandishi...,
 
Vyote hivyo alikuwa navy vya nini???
Kuna deal imeharibika mahali?
 
mh! Maswali ni mengi lakini hatutakaa kupata majibu, ila hii hali ichangie kuwafahamu viongozi waliopewa dhamana ya uwaziri! Verrry changamoto
 
Back
Top Bottom