Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
KAMPALA- Polisi bado wanaendelea kutafuta watu ambao wanaaminika kufunikwa na kifusi kwenye jengo lililo anguka maeneo ya Makindye jijini Kampala Ijumaa ya Septemba 11 ,2020 majira ya saa mbili usiku.
Mtu mmoja aliyefahamika kama Godfrey Oonyu ambaye ni mwalimu aliyekua akifanya kazi katika jengo hilo baada ya shule yake kufungwa kufuatia ‘lockdown ‘ inayoendelea nchini humo ameokolewa na maafisa wa polisi.
Oonyu amesema kuwa takribani wenzake 8 wamenaswa chini ya kifusi, huku mmoja wa wahanga aliyefahamika kwa jina moja pekee la Alex ambaye ana aminika kuwa bado amenaswa chini ya kifusi, alimpigia simu dada yake mnamo saa tano na nusu usiku akiomba msaada.
Ila mpaka sasa hajapiga tena simu.
Jitihada za kuchimba usiku zilikua hafifu kwakua waliojitokea kufanya hivyo walikua wakitumia nyenzo zisizo imara kama vile majembe, mashoka na nyundo.
Asubuhi ya leo Jumamosi ya Septemba 12 ,2020 polisi wamepeleka vifaa imara kwa ajili ya uchimbaji.
Msemaji wa polisi wa Kampala Bwana Onyango ameeleza kuwa jengo hilo linamilikiwa na mfanyabiashara aliyefamika kama Kagolo ambaye anafanya kazi kwenye Kikuubo Lane ambacho ni kitovu cha biashara katikati ya mji.
“Afisa wetu ambaye alitembelea eneo la tukio aligundua kuwa kuna uhalifu wa kuharakia na uzembe.
Maafisa wawili wa mamlaka ya mji mkuu wa Kampala ambao walipaswa kusimamia mradi wa ujenzi wa jengo hilo wamekamatwa “ Alisema Onyango .
Maafisa wa mamlaka ya mji mkuu wa Kampala(KCCA) waliowekwa kizuizini kwenye kituo cha polisi cha Katwe ni ;Bi Anne Achoma, Bwana Joseph Balikuddembe.
Bwana Onyango amesema kuwa ujenzi ulikua unaendelea bila mipango iliyoidhinishwa.
“ Walienda (maafisa) eneo la ujenzi wakawapa maelekezo ya kusimamisha ujenzi, lakini baadaye, waliondoa taarifa hiyo na kuwaruhusu waendelee na ujenzi huo “ aliongeza Onyango.
Mnamo mwezi May jengo lingine ambalo lilikua chini ya matengenezo maeneo ya Lukuli Makindye lilianguka na kuuwa zaidi ya watu 12.
KCCA officials detained over collapsing Makindye building