Maafisa wa serikali wanapowajibishwa, na misingi ya kidemokrasia inapoheshimiwa kuna uwezekano mkubwa wa huduma za umma kuboreshwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kwa maana ya jumla, kwa watu wengi duniani, demokrasia maana yake ni nguvu ya wengi katika kufanya maamuzi yanayohusu
umma na kuweka usawa wa kisiasa katika matumizi ya nguvu hiyo (International IDEA 2008: 20-21).

Demokrasia ni lazima iwape wananchi uwezo wa kujieleza na kuwasilisha hoja zao kwa utaratibu mzuri unaowafikia wawakilishi wao. Wazo la msingi ni kwamba kuwepo kwa mifumo ya uwajibikaji katika demokrasia kuhakikisha maafisa wa serikali wanatoa huduma za viwango vya juu kabisa kwa watu, vinginevyo wanawajibishwa ipasavyo ikiwa hawatafanya hivyo.

Maafisa wa serikali wanapowajibishwa, na misingi ya kidemokrasia inapoheshimiwa na kufuatwa kuna uwezekano mkubwa wa huduma za umma kuboreshwa, kwa haraka, kwa wakati muafaka, kwa ubora wa juu au kutekelezwa vizuri zaidi.
 
Vipi kwa uzoefu wako, demokrasia tuliyopitia awamu 5 ya mkono wa chuma ina mchango gani katika maendeleo ya nchi? Ni mfano wa kuigwa au lah?
 
Kwa maana ya jumla, kwa watu wengi duniani, demokrasia maana yake ni nguvu ya wengi katika kufanya maamuzi yanayohusu
umma na kuweka usawa wa kisiasa katika matumizi ya nguvu hiyo (International IDEA 2008: 20-21).

Demokrasia ni lazima iwape wananchi uwezo wa kujieleza na kuwasilisha hoja zao kwa utaratibu mzuri unaowafikia wawakilishi wao. Wazo la msingi ni kwamba kuwepo kwa mifumo ya uwajibikaji katika demokrasia kuhakikisha maafisa wa serikali wanatoa huduma za viwango vya juu kabisa kwa watu, vinginevyo wanawajibishwa ipasavyo ikiwa hawatafanya hivyo.

Maafisa wa serikali wanapowajibishwa, na misingi ya kidemokrasia inapoheshimiwa na kufuatwa kuna uwezekano mkubwa wa huduma za umma kuboreshwa, kwa haraka, kwa wakati muafaka, kwa ubora wa juu au kutekelezwa vizuri zaidi.
Mmeanza kuamka usingizini. Hamjachelees Unagana na watanzania wote kupigania Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom