Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
Maafisa wa usalama Kenya wakishika doria katika jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC). Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) ukiongozwa na Raila Odinga umepanga kuandamana hadi kwenye afisi hizo zilizo karibu na Chuo Kikuu cha Nairobi kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti. Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba lakini Nasa wanasema sharti mabadiliko yafanywe kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika uchaguzi huo.