Maafisa wa usalama Kenya wakishika doria katika jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za (IEBC).

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,281


Maafisa wa usalama Kenya wakishika doria katika jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC). Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) ukiongozwa na Raila Odinga umepanga kuandamana hadi kwenye afisi hizo zilizo karibu na Chuo Kikuu cha Nairobi kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti. Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba lakini Nasa wanasema sharti mabadiliko yafanywe kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika uchaguzi huo.

 

Attachments

  • FB_IMG_1506414868266.jpg
    51.4 KB · Views: 30
  • FB_IMG_1506414872203.jpg
    59.6 KB · Views: 29
  • FB_IMG_1506414870273.jpg
    56.2 KB · Views: 27
  • FB_IMG_1506414876207.jpg
    53.6 KB · Views: 29
Mmmh mkuu inatisha, polisi wetu wakipata mavazi kama hayo ujuwe tumekwisha
 
Nakubaliana na alivyosema Jaji Lubuva
 
Kabla ya kutekwa, kuteswa na kumuua jamaa wa IEBC hakukuwa na ulinzi wowote.
Inamaana walidhamiria kumtoa roho yule jamaa..!
 
Basi wanafiki wapinzani wa bongo ingekuwa kwetu ungesikia wanaropoka eti mara polisi CCM.
 
Basi wanafiki wapinzani wa bongo ingekuwa kwetu ungesikia wanaropoka eti mara polisi CCM.
Wale wanalinda tu ofisi ya uma, hawajaenda kumshusha Raila jukwaani kama wa kwetu walivyoenda kumshusha Msigwa kule Iringa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…