tunasema tu! Mnakumbuka issue za new millenium ? Yaani tulipokuwa tunaingia mwaka 2000 kutoka 1900. Nilikuwa Arusha basi maneno Mengi yalikuwa yakizungumzwa wataalam wakitudanganya kwamba computer zitavamiwa na millenium bug na hazitafanya kazi tena! Pale Sekei watu wanadanganyana eti mlima Meru utakuwa covered na theluji Kama Kilimanjaro.
Issue kubwa ilitokea Moshi mjini siku ya mkesha wa mwaka mpya. YMCA club wana yale mataa yanamulika juu sasa siku hiyo wakaanza mambo mapema Kama saa nne hivi usiku mataa si yanamulika anga basi raia kuona mawinguni mwanga unatokea unapotea daaah watu waligonga kengele makanisani watu mbiooo makanisani Yesu anarudi. Kumbe vidosho na bwana zao wanakula bata pale YMCA. mie nawaaambia kuwe giza dk tano tu saa sita mchana tutapoteza Watu wengi sana including mtoa mada hahaha