Maajabu: Magufuli anataka tuwe na Club ya Taifa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
"Bashungwa tumekupeleka kwenye michezo tunataka tushinde, sio tukilala tukiamka mabao 10, wote mtaondoka hata wewe Naibu Waziri Ulega, tukashinde, na Simba na Yanga zimetuchelewesha ikiwezekezana tuwe na Club ya Taifa kabisa isiyokuwa na Usimba na Yanga” asema Rais Magufuli akiwaapisha Mawaziri wapya leo IKULU Dodoma.
 
Mpira kwasasa kuna vitu vingi ilikupelekea mafanikio labda ajiulize, kwanini timu za taifa nyingi maendeleo yao sio mazuri?

Jibu ni masilahi katika timu zao wanazolipwa hela vingi hivyo upelekea wachezaji kutokuwa na morali katika timu za Taifa. ( Kwasababu tu hakuna hela za kutosheleza)

Na hili tatizo hata wazungu wanalijua!! Jingine la mwisho kabisa kwa timu pale TFF lakini hakuna impact yoyote katika timu yetu ya Taifa, ni kwasababu watoto wa pale TFF wanacheza kwa kujuana na viongozi.

NB , Senegal mwaka 2002 walifanya maajabu katika Kombe la dunia sio kwa maajabu walijipaga , ndio maan waliwapeleka vijana nchini France wote kwa pamoja.

Mpira sio siasa , mpira sio nguvu mpira unahija akili.
 

SimBa na yanga ndizo zina kwamisha virabu vya hapa na mpira
 
Suluhu kubwa, ni UWEKEZAJI WENYE TIJA!! SERIKALI INAPASWA KUWEKEZA KWENYE MPIRA
 
Club ya taifa,,ni wazo zuri,itawajibika kwa waziri muhusika na hii haitakiwi ifungwe labda draw tu
Sasa hii club itaundwa vipi? Mwenyekiti wake atakuwa waziri? Usajili wake itafanya vipi? Maana siamini kama club ya taifa itanunua wachezaji Kenya. Huo sio uzalendo. Watavaa jezi gani? Itaitwa jina gani? Bashungwa ana kazi kama yule aliyeambiwa aanzishe historia ya Tanzania.
 
Club ya Taifa lazima itachukiwa na wapinzani wote pamoja na wale waliotumbuliwa majipu.
Wizara ijikite na kuzisaidia timu za Taifa na kuhamashisha uzalendo wa kuzishabikia timu zote zinazowakilisha nchi

Pia kuwe na mpango mkakati wa muda mrefu. Mfano kuwatafutia timu ulaya wachezaji wote wa timu ya taifa ya vijana (serengeti boys) ili wakalelewe huko. Baada ya miaka mitano tutakuwa na timu ya taifa inayojimudu. (Tukajifunze walivyofanya Madagasca)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…