Maajabu matokeo kidato cha nne
MATOKEO ya kidato cha nne yaliyotangaza hivi karibuni yameendelea kuibua mkanganyiko kutokana na kuwapo kwa utofauti wa madaraja kwa pointi zinazozolingana.
Mkanganyiko huo unatokana na kuwepo kwa hali ya sintofahamu kutokana na kutoeleweka ni kigezo gani cha kutofautisha matokeo hayo kimetumika.
Katika matokeo hayo kuna wanafunzi wana-alama (points) 42 wamepewa daraja 0, na kuna wanafunzi wana pointi 46 wamepewa daraja la IV.
Pia kuna waliopata points 43 wamepewa daraja la IV na wengine wamepata points 43 wamepewa daraja 0
Mfano wa matokeo hayo ni shule ya sekondari Wigamba ya Mbeya. Namba za mtihaniwa na pointi alizopata na daraja zikiwa kwenye mabano ni S3133/0088 (45- iv), S3133/0082 (45- 0), S3133/0092 (42-0), S3133/0095 (43-0), S3133/0099 (44-0), S3133/0100 (42-iv), S3133/0101 (43- iv) na S3133/0103 (44-iv)
Shule nyingine ya Nchimbi ambayo matokeo yake ni S1877/0001 (43-iv), S1877/0003 (43-iv), S1877/0006 (46-iv), S1877/0007 (46-iv),
S1877/0028 (44-iv) na S1877/0037 (45-0)
Wadau wa elimu wanahoji kuwa ni kigezo kipi kimetumika kuchukua mfumo huo wa kupanga matokeo.
Bavicha: Matokeo kidato cha nne ni ya kisiasa
Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) limesema matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa na serikali juzi ni ya kisiasa zaidi.
Katibu Mkuu wa Bavicha, Deogratias Munishi, alibainisha hayo jana na kuongeza kuwa serikali imejinasibu kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 15.17 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana huku ikiwa yako kisiasa zaidi na yanashindwa kuakisi ukweli wa hali ya elimu nchini.
Alisema matokeo hayo yameendelea kuonyesha jinsi mfumo wa elimu nchini ulivyoharamu kwa vijana, kwani kundi la wanafunzi waliofanya mtihani huo ni wale waliomaliza darasa la saba mwaka 2009.
"Wanafunzi takribani 898,420 wameshatupwa nje ya mfumo kwa kati ya 2009 na 2013, kwani waliotarajiwa kumaliza darasa la saba 2009 walikuwa 1,024,488 huku 502,624 wakifeli vibaya, 493,333 wakidaiwa kufaulu na 28,531 wakiwa haijulikani wamepotelea wapi na hadi wanafunzi 404,083 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2013 maana yake wanafunzi 89,250 walishapotelea njiani leo hii wanaleta siasa," alieleza Munishi.
Alisema Bavicha wanaendelea kusisitiza kuwa kuna anguko kubwa la kiwango cha elimu nchini na matokeo mabovu ya mtihani wa taifa kila mwaka ni kielelezo kikuu cha anguko hilo.
"Serikali imeshindwa kuwekeza vya kutosha kwenye sekta hii kwa kuweka miundombinu na mazingira wezeshi ya kutoa elimu bora kwa raia wake na kuonyesha upofu wa kuendelea kukumbatia mfumo mbovu," alisema.
Aliishauri serikali kuachana na anasa katika matumizi ya rasilimali za nchi, ili iwekeze katika elimu.
Pia kuwepo na udharura wa kushughulikia mabadiliko ya mfumo wa elimu, ili kupata taifa la wasomi na si kama ilivyo hivi sasa, ili kunusuru kizazi kilichopo na kijacho.
Pia wamemtaka Waziri Mkuu kuanika ripoti ya tume aliyoiunda mwaka jana kuchunguza matokeo mabovu ya wakati huo.
Source - Tanzania Daima