Maajabu matokeo ya kidato cha sita 2018

Maajabu matokeo ya kidato cha sita 2018

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Unaweza kuyaita maajabu ya aina yake baada ya Baraza la Mitihani Taifa (Necta), kutangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018, huku shule kongwe ya Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa katika orodha ya shule 10 za mwisho.

Jingine katika matokeo hayo ni Shule ya Sekondari Kibaha kupanda kwa nafasi 10 na kuwa shule ya kwanza kitaifa. Katika matokeo ya mwaka 2017 shule hiyo iliyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani ilishika nafasi ya 10.

Akitangaza matokeo hayo jana, mjini Unguja, katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema ufaulu wa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 1.52 baada ya watahiniwa 83,581 kufaulu sawa na asilimia 97.58. Mwaka 2017, watahiniwa waliofaulu walikuwa 70, 552 sawa na asilimia 96.06.

Alisema watahiniwa wasichana wameongoza kwa ufaulu kwa kupata asilimia 98.26 dhidi ya wavulana waliopata asilimia 97.12.
Kwa upande wa watahiniwa binafsi, alisema waliofaulu ni watahiniwa 8,276 sawa na asilimia 88.35 ya watahiniwa 9,371 waliofanya mtihani huo Mei, mwaka huu.

Siri shule 10 bora

Kama ilivyokuwa katika mtihani wa mwaka 2017, shule zilezile za Serikali zilizofanya vizuri mwaka huo ukiondoa Tabora Boys, mwaka huu zimeelezwa kuingia tena katika orodha ya shule 10 bora ambayo bado imeendelea kutawaliwa na shule binafsi. Shule hizo ni Kibaha (nafasi ya kwanza), Kisimiri (nafasi ya pili) na Mzumbe (nafasi ya nne).

Shule nyingine katika orodha hiyo na nafasi zake kwenye mabano ni Kemebos (3), Feza Boy’s (5), Marian Boys (6), Ahmes (7), St Mar’ys Mazinde Juu (8), Marian Girls (9) na Feza Girls (10).
Akieleza mafanikio ya Shule ya Sekondari Kibaha kufanya vizuri, mkuu wa shule hiyo, Chrisdom Ambilikile alizitaja sababu kuu mbili zilizoibeba ambazo ni mipango mizuri pamoja na juhudi za walimu.

“Mara kwa mara tunaingia kumi bora kitaifa, lakini safari hii Mungu mkubwa tumeshika nafasi ya kwanza kitaifa. Kingine ni ushirikiano wetu na wazazi kupitia kamati zao. Pia wanafunzi kuwa na nidhamu,” alisema.
Mkurugenzi mkuu wa Shule za Feza Tanzania, Ibrahim Yunus alitaja siri ya mafanikio ya shule hizo kuwa ni ushirikiano uliopo baina ya uongozi, walimu na wazazi.

Alisema kila siku wanafanya tathmini ya shule zao na kuweka mikakati ya kuendelea kutoa elimu bora.
“Matarajio yetu ni kuendelea kufanya vizuri zaidi. Tunajitahidi kuwa mfano wa elimu bora hapa nchini,” alisema Yunus na kusisitiza kwamba, shule za Feza zinazingatia zaidi ubora wa elimu.

Mkurugenzi huyo alizipongeza pia shule za Serikali ambazo mwaka huu zimeingia kwenye kumi bora na kusisitiza kwamba wanafunzi wote ni Watanzania, hivyo wanahitaji elimu bora bila kujali wanasoma shule binafsi au za Serikali.

Kwa upande wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian, mkuu wa shule hiyo, Lightness Massawe alisema siri ya kuingia katika orodha ya shule 10 bora ni kujituma na kuwajenga wanafunzi wao kinidhamu.
Sababu kama hizo pia zilitajwa na mkuu wa Shule ya Wavulana ya Marian, Ihonde Joseph huku akiongeza nyingine kuwa ni kuwajengea wanafunzi wao uwezo wa kujitambua.

“Tulifanikiwa kwa sababu wanafunzi wote walikuwa kitu kimoja na lengo lilikuwa moja ambalo ni kusoma kwa bidi,’’ alisema Joseph.
Akizungumzia mafanikio ya shule yake, mkuu wa Sekondari ya Kisimiri iliyopo mkoani Arusha, Valentino Tarimo alisema siri ni ushirikiano mzuri baina ya walimu, jamii na wanafunzi ambao kila mwaka hushindana kuvunja rekodi ya mwaka uliopita.

Alisema walidhamiria kushika nafasi ya pili kitaifa katika matokeo ya mwaka huu.
“Wanafunzi wetu wamekuwa wakishindana wao kwa wao kila mwaka kufanya vizuri na hii ndio siri kubwa,” alisema Tarimo
Pia alisema ushirikiano uliopo baina ya jamii inayozunguka shule, walimu, Halmashauri ya Meru na wanafunzi umekuwa ukiongeza ari ya wanafunzi kufanya vyema.

“Hapa sisi wanafunzi wetu kwanza likizo ndefu muda mwingi wapo shule, tunawapa siku saba tu lakini pia wakiwa shuleni muda mwingi ni kusoma,” alisema.
Alisema mikakati ya uongozi wa shule ndio imeifanya shule hiyo tangu ianzishe kidato cha tano mwaka 2006 kuwa ndani ya 10 bora.

Tarimo alisema hata katika matokeo ya kidato cha nne tangu shule kuanzishwa mwaka 2002 wamekuwa wakifanya vizuri.

“Tunajivunia mafanikio haya na inaonyesha shule za kata zinaweza kufanya vizuri sana,” alisema.
Jangwani ndani ya 10 za mwisho
Pamoja na shule hizo tatu kuitoa Serikali kimasomaso, bado kwa upande mwingine imepata pigo baada ya Shule ya Sekondari Jangwani kutajwa kuwa miongoni mwa shule 10 za mwisho. Kinachoshagaza ni hadhi na hata umaarufu wake kitaaluma tangu ianzishwe mwaka 1928.

Katika matokeo hayo, wanafunzi 20 walipata daraja sifuri, 11 walipata daraja la nne na wanafunzi 83 daraja la tatu. Wanafunzi waliopata daraja la pili ni 25, huku mwanafunzi mmoja pekee akipata daraja la kwanza.
Mkuu wa shule hiyo, Geraldine Mwaisenga hakuwa tayari kueleza sababu ya shule yake kuwa ya vibaya, licha ya kuonekana kushtuka na kutoamini baada ya mwandishi wa Mwananchi kumtajia matokeo ya shule yake.

Awali gazeti hili lilifika shuleni hapo na kukutana na baadhi ya walimu ambao hata walipoombwa kuelekeza alipo mkuu huyo wa shule, walikataa kwa madai kuwa alikuwa ametingwa na wageni
Hata hivyo, baada ya kutafutwa kwa simu ya mkononi alijibu kwamba yupo eneo la shule, lakini asingeweza kuzungumza na vyombo vya habari kwani alikuwa na kazi ya ukaguzi wa majengo.

“Kwa sasa tunafanya ujenzi na ukarabati wa majengo, hivyo nipo na wageni. Hata hivyo kwa leo siwezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa bado sijaona matokeo yenyewe,” alisema Mwaisenga.
Baadhi ya wanafunzi ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini walisema watahiniwa wa mwaka huu walionyesha dalili mbaya tangu mapema.

“Kwa kweli tumejisikia vibaya. Kidato cha sita waliopita walikuwa wazembe, hawakujituma kusoma na hata matokeo yao ya mitihani ya majaribio hayakuwa mazuri,” alisema mwanafunzi mmoja.
Matokeo ya Jangwani yamekuja miaka miwili baada ya shule nyingine kongwe ya Azania nayo kufanya vibaya katika matokeo ya mwaka 2016.

Sayansi yaiangusha Golden Bridge

Shule iliyoshika mkia katika matokeo hayo ni Golden Bridge ya mkoani Geita.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Juma Malunga alisema kwa njia ya simu kuwa wanafunzi wake wameangushwa kwa kutomudu masomo ya sayansi, huku akikiri kuwa walisajili wanafunzi kusomea masomo hayo wakiwa na ufaulu mdogo.

Soma Pia Matokeo mengine kuanzia 2009

“Wanafunzi wangu wengi ni wale waliomaliza shule za kata na matokeo yao ya kidato cha nne hayakuwa mazuri. Hili limekuwa funzo kwangu, sitapokea wahamiaji wala waliopata ufaulu wa alama CCD. Ni bora niwe na wanafunzi wachache wazuri kuliko wengi watakaofeli,” alisema.

Matokeo ya mwaka 2017

Mwaka 2017 shuele ziizoongoza ni ni Shule ya wasichana ya Feza (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Kisimiri (Arusha), Ahmes (Pwani), Marian Girls (Pwani) Mzumbe (Morogoro), St Mary Mazinde Juu (Tanga), Tabora Boys (Tabora), Feza Boys (Dar es Salaam) na Kibaha (Pwani).
Shule zilizoshika mkia ni Kiembesamaki ya Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam), Ben Bella (Unguja), Meta na Mlima (Mbeya), Al-Ihsan Girls (Unguja) na St Vicent (Tabora).

Mwaka 2016

Shule zilizoongoza ni Kisimiri (Arusha), Feza Boys (Dar es Salaam), Alliance Girls (Mwanza), Feza Girls (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Tabora Boys (Tabora), Kibaha (Pwani), Mzumbe (Morogoro), Ilboru (Arusha) na Tandahimba (Mtwara).
Zilizofanya vibaya ni Mpendae, Ben Bella, Tumekuja, Green Bird Boys, Jang’ombe, Kiembesamaki, Tanzania Adventist, Ala-Ihsan Girls, Azania na Lumumba.

Mwaka 2015

Feza Boys (Dar es Salaam), Runzewe (Geita) Feza Girls (Dar es Salaam), Sumbawanga (Rukwa), Ivumwe (Geita), St Mary’s Mazinde Juu (Tanga), Vwawa (Mbeya), Kisimiri (Arusha), Namabengo (Ruvuma) na Scolastika (Kilimanjaro).

Zilizofanya vibaya ni Meta (Mbeya), Kwiro (Morogoro), Mtwara Tech (Mtwara), Iwanje (Mbeya), Lugoba (Pwani), Kaliua (Tabora), Kilangalanga (Pwani), Lwanga (Mbeya), Ilongero (Singida), Bariadi (Simiyu)
 
Watanganyika hamna jema nyie. Sasa hivi kila mkuu wa shule ya serikali anakomaa na wanafunzi wake na shule yake ili ifanye vizuri kulinda chakula chake, nan anakubali shule yake iwe ya mwisho kirahisirahisi ili atumbuliwe. Sasa hivi wanafunzi wanasoma na kukaziwa haswa huko mashulen. Haswa boarding. Pongezi kwa serikali
 
Ningekuwa mkuu wa shule asee wanafunzi wangu wangesoma hata na meno
 
Hivi jangwani hatuwezi kuihamishia msata? naona mazingira sio rafiki kwa wanafunzi, hilo eneo tuwape azam wawekeze
 
Back
Top Bottom