Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Habari kamili hii hapa
Mtangazaji Burton Mwemba, maarufu Mwijaku ameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwa na mfumo mzuri wa kuangalia aina ya upatikanaji viongozi kwa baadhi ya nafasi hasa zile za kuteuliwa na Rais au taasisi fulani.
“Kumteua mtu lazima kuwe na utaratibu wa aina mbili kwanza kwa kuangalia historia yake kwa kuzingatia anachokwenda kukifanya, wengi wanaingia kwenye siasa si eneo lao mtu amesoma kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne hajawahi kuwa kiranja.
“Amekuja chuo hajawai kuwa kiongozi anakuja mbele anajua kuongea anaonekana na anapewa nafasi ya U-DC (mkuu wa wilaya) matokeo yake anashindwa kuchagua maneno ya kuzungumza, lakini tukitengeneza mfumo hata akichaguliwa na taasisi fulani tunarejea historia yake aliwahi kuwa hata kiranja?
Mwijaku amesema hayo leo Jumatano Septemba 4, 2024 wakati akichangia mada kwenye Mwananchi Space, inayoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL), inayosema: Kauli tata za viongozi kuelekea kwenye uchaguzi zinatafsiri gani?
“Tunapaswa kutambua viongozi wengi ni wateule kutoka kwa Rais anayewapa mamlaka na waliowengi wabinafsi anapoona hapati nafasi ya kuwa karibu na kiongozi fulani ndipo tunaanza kuona matamshi ambayo si mazuri kwa chama na Serikali yake.”
Katika hoja yake ya pili, Mwijaku amependekeza ni muhimu kuangalia uwezo wake wa kufikiri kuna kauli zinaweza kutolewa na kiongozi na kubaki na maswali ya kujiuliza ni kiongozi au chawa?
Soma Pia: Serikali Kuja na Mfumo Maalumu wa Kusaidia mamlaka ya Uteuzi kufanya uteuzi kwa Usahihi
“Ni muhimu tujue kutofautisha kati ya chawa na kiongozi, chawa anaweza kukaa na kusifia chochote lakini kiongozi akitoa kauli ajue ni uamuzi wa Serikali kwa kuwa umepewa sehemu ya kuwakilisha.