Maajabu:Pesa za TASAF zapigwa kwa ajili ya ziara ya Mbunge

Maajabu:Pesa za TASAF zapigwa kwa ajili ya ziara ya Mbunge

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
IKUNGI-SINGIDA


Katika hali isiyokuwa ya kawaida kuna taarifa kutoka jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida kwamba Mbunge wa jimbo hilo Miraji Mtaturu ameshirikiana na baadhi ya viongozi wa Kata ya Ntuntu katika Wilaya ya Ikungi kukata pesa kwa ajili ya kunusuru kaya maskini almaarufu kama TASAF kwa ajili ya kuandaa ziara yake.

Kwa taarifa za kutoka kwa mnyetishaji wetu ni kwamba kila mwananchi amekatwa shilingi 10,000 bila ridhaa yao. Inaelezwa kwamba wananchi hao maskini wamelazimishwa kukubali kukatwa bila kuridhia wenyewe.Kitendo hiki kimelalamikiwa sana na wananchi wengi katika wilaya hiyo.

Wameomba mamlaka za juu ikiwemo TAKUKURU kufuatilia jambo hilo ili watoe ufafanuzi kama ni haki wananchi hao maskini kukatwa pesa hizo bila kuridhia. Wamedai kama lengo ni kunusuru kaya maskini imekuaje zigeuzwe kua kama mradi wa mbunge? Lengo lake lililokusudiwa lilikua kufanyia ziara ya mbunge?

Mbaya zaidi inaelezwa kwamba hizo pesa ni watu wachache wameingiza ziara ya mbunge ili waweze kujigawia hizo.
 
Back
Top Bottom