Maajabu ya biashara ya uchimbaji wa madini ya dhahabu

Shida wachimbaji wengi wanatokea kwenye jamii zinazoamini ushirikina kwenye kila Jambo...wasukuma na Kanda ya ziwa...Ila ushirikina haina NAFASI kabisa...NI kumaliza ndugu na watoto...
 
Sio ushirikina ni mila na desturi za jamii za kiafrika,kabla hujawa brainwashed na dini za mashariki ya kati,bure wa head.
 

Achana na wasukuma wanaotumia Imani kwenye uchimbaji. Uchimbaji ni sayansi. Watu wanawekeza mabilion kwenye utafiti Ili apate madini mtu anakuja kuleta story za Imani.


Kwa taarifa tu utafiti ni ghali kuliko hata kuchimba kwenyewe. Ila sisi tunawekeza kwenye kuchimba zaidi ya utafiti.


Kuna kampuni nyingi za wazungu wanavuna Rare Minerals HUWEZ kusikia wanabahatisha. Ni wamewekeza kwenye tafiti so wako actual.


Tembelea tume ya madini Huwa wanauza vitalu Kwa bei nafuu sana ambavyo vimeshafanyiwa tafiti.


Fungua full plant na weka CIL Machine walau wa kusaga Tani 20 Kwa saa.


Nunua Howo walau 3

Excavator walau 1


Wheel loader 1


Na vifaa vingine.



Huo ni uwekezaji mkubwa si mchezo.


Mambo ya kuchimba madini ukiwa na mifupa ya fisi mfukoni ni ushamba wakati wachina wanakuja hapa na machines wanaondoka na dhahabu kama zote.



Unaweza kuwapitia Hawa EcoGraf


Soma investment waliyofanya halafu linganisha na investment za watanganyika wao wanaishia kwenye Kununua uchawi tu.


Hao wa Australian construction ya site tu ( mradi mzima ) ni Dola milion 58... Zaidi ya bilion 100 dadeki
 
naunga mkono hoja utafiti wanaofanya ni mabilioni ya dola na ukishalipa leseni kitalu kinakuwa chako kuna wachina niliwadodosa..wanasema baadhi ya vitalu dhahabu ni ndogo kuliko uwekezaji watakaoufanya kwa bei ya dhahabu kwa sasa kuichimba ni hasara kwa hio wanakwenda palipo na dhahabu nyingi zaidi ila wabongo wanavyopakomalia na kumaliza mitaji ni aibu...utasikia fedha ya dhabu mpaka uagwe na babu.wakati ni hesabu tu...
 
Uzi mzuri sana huu umetoa siri ambazo wengi tulikuwa hatujui.
Je kwa maoni yako unamshauri nini mtu ambaye anataka kujiingiza kwenye hiyo biashara ya madini kuanzia uchimbaji hadi uchuuzi wa madini?
Na mtaji anatakiwa awe na pesa ngapi ili biashara iende vizuri?
 
Reactions: apk
Njoo huku kanda ya ziwa uone wachimbaji wanavyopendezesha mji
Wana ma gest ma hotel majumba ya kufa mtu

Gali zao pendwa za polini ni Kluger za kutembelea ni VXV8
 
Nakupata sana yani swala kuwekeza wataalamu mtu yupo bora kuwekeza waganga.
Acha nitunze maeneo yangu ambayo PPm bado inanipa matumaini mpaka nikamilishe vibari.
Dhahabu haipo hivyo mkuu, kiuhalisia ukitumia gold detector unaweza usipate hata mia tofauti na ndumba

Kama nasema uongo waulize vijana wa mining UDSM waliokimbilia huko machimboni
 
wtu mnapenda kuuliza maswali ya kijinga sana....unataka kuingia kwenye biashara ambayo hujui bei ya bidhaa sokoni fanya utafiti kilo moja sasa ni sawa na m250tzs lakini kuna watu wanafanya kwa mtaji wa laki 5 hio biashara...au chini ya hapo kabisa..cha muhimu unajua unachokinunua..unajua kinauzwaje na dhamani yake sokoni....ukifika field unakuta wachimbaji ni wajuzi kuliko wewe unauziwa mabati na maudongo unarudi na ni ngumu kutoboa
 
Mkuu wewe huamini uchawi katika uchimbaji wa dhahabu?
Hakunaga uchawi, cha muhimu ni technology tu! Kinachofanya mchimbaji mdogo kuamini uchawi ni kwasababu wanabahatisha wanachimba bila kujua mkanda wa dhahabu uko wapi, mzungu mwenye technology anafanya exploration anajua madini kwa urefu upi nitayakamata, anaweza chimba mita80 kwenda chini akitafuta njia ya kuingilia ili afike madini yalipo na anajua yapo kiasi gani, atachimba kwa muda gani hadi kuishi, ila mchimbaji mdogo akifika mita30 anaenda kwa mganga amtabirie kimazingaombwe yale ya kubahatisha! Ndo kuanza kuambiwa kalete titi moja la Nicole, kalete kichwa chenye upara, sijui kalete nyeti za mtotoπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ kaue mwanao wa kwanza kumbe madini kayaacha kushoto kachimba kulia
 
Dhahabu haipo hivyo mkuu, kiuhalisia ukitumia gold detector unaweza usipate hata mia tofauti na ndumba

Kama nasema uongo waulize vijana wa mining UDSM waliokimbilia huko machimboni
NIPO HUKO NAELEWA NA SIFANYI HIZO ZA MTINDO HUO NAPELEKA MAABARA KUPIMWA NA KUFANYIA UCHAMBUZI.
 
Reactions: apk

Hii biashara ni nzuri pia ukiwa mnunuaji wa madini kutoka kwa wachimbaji unakuwa hauko katika risk​
Hapa ndio mimi nahitaji kupata darasa jinsi gani ya kuanza hii biashara,mtaji wa kuanzia ni kiasi gani,pa kununulia ni wapi,soko la kuuza ni wapi.
Na cha muhimu zaidi najilinda vipi na utapeli wa kwenye madini,pia nawezaje kuyajua madini feki na halisi.
Msaada hapa
 
Nipe ABC mkuu kuliko kunikatisha tamaa mpunga ninao wa kutosha ninachozungumzia hapa teknolojia kulipa wafanyakazi kwangu sio shida


Ukute una ka-milioni 100 kako unadhani Una Hela nyingiii, Teheee!!

Ndg.,
Biashara Si-ya Dhahabu pekeyake na ya Madini yoyote yale,
Si kwamba inahitaji Pesa nyingi pekeyake.
Elimu ni muhimu kabla ya kuianza Biashara yenyewe.
Kuna mdau kasema toka, katembee Saiti na isiwe sehemu moja tu,
Hilo ndio la msingi na sekondari kupita maelezo yoyote atakaekupa yeyote yule.

Endelea kuagiza taarifa ukiwa hapo kwenye Sofa likukute jambo.

Nawasilisha.
 
Technology inatofautiana, kuna zile machine zenye uwezo mdogo ambao haufiki mbali, za kuuzwa milioni 6_15 ufanyaji kazi wake mmhh huwa ni wa kubahatisha, company kubwa kubwa wanatumia technology ya billions of money ili kujua wanafanya nini, kwa mfano kama exploration inatumia billions of money zile equipments wanazotumia kupimia uoatikanaji wa dhahabu na kujua how far ni za pesa mingi ambayo mchimbaji mdogo ukute hata mtaji uliopo haufiki robo ya kifaa cha kupimia ardhini.
Pesa lazima ikate
 
Sina uzoefu kwa migodi ya tz ninauzoefu wa migodi ya nje kama Congo mozombiqu
So sio mgeni kwenye kipengele cha dhahabu naongelea uwekezaji wa Tanzania
 
Samahani nilikuwa nataka kujua naweza kuanza na mtaji wa shs kwenye hii biashara ya dhahabu? maana naipenda sana nataka nianze hii biashara maana naona unasema ni elimu tu hata mtaji mdogo unatosha?? naomba unisaidie
 
Reactions: apk
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Mwakitoryo ulikuwa namba ngapi nimechimba sana namba 2 na namba 3 baadae nikaondoka zangu ila nasikia siku hizi wachina wametapakaa vibaya mno. Dutwa na Nyarugusu nilikaa ila sikuwahi kuzidisha wiki kwenye hayo machimbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…