Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Asubuhi saa 12 taarifa ya habari Magic FM wameripoti kuwa zaidi ya wanafunzi 2000 kati ya 4000 watakaofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu wilani Karambo mkoani Rukwa, hawajui kusoma na kuandika. Sasa najiuliza watafanyaje mtihani wakati hawajui kusoma na kuandika? Na je walipitaje toka darasa la kwanza mpaka la saba wakiwa hivyo? Na kama wamegundulika hivyo ni kwanini wakubaliwe kufanya mtihani wa darasa la saba?
Ikumbukwe pia miaka miwili iliyopita serikali ilikiri bungeni kuwa zaidi ya wanafunzi 5200 walifaulu kuingia kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Maana yake ni kuwa hawa sasa wako kidato cha tatu. Na kwakuwa tumepunguza madaraja ya ufaulu ili kupata idadi kubwa ya "wasomi", hawa nao "watafaulu tu!" Maswali ni kuwa: Walifauluje? Na wanafanya nini sekondari? Na kwanini serikali imeruhusu hali hiyo? Je lengo ni kuwa na takwimu kubwa kupita ubora? Hivi serikali ipo na inaona? Hii elimu yetu inaelekea wapi?
Unaweza kushangaa hawa wanaofaulu wakiwa hawajui kusoma na kuandika wakaja wakawa marais wetu, mawaziri, madaktari, wanasheria nk nk Hapo ndipo tutakapo kiona cha mtema kuni. Kwa mtindo huu wa kuwa "wapite tu" si ajabu tunao watu wa aina hiyo ndani ya system ndio maana tunashuhudia mikataba ya ajabu na kauli za ajabu kwa viongozi wakubwa kabisa serikalini. Ndipo utashangaa kiongozi anatoa taarifa katika mkutano wa kimataifa kuwa Tanzania ni muungano wa visiwa vya Zimbabwe na Tanganyika mwaka 11964. Na kuthibitisha wengi ndani ya utawala wako hivyo hakuna anayeona na kuchukua hatua. Ukienda mbele kidogo utakutana na msomi mwingine wa uchumi atakwambia hajui sababu za kwanini nchi anayoiongoza ni masikini! Naona giza mbele!