Maajabu ya khanga!

Bitoz

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
30,823
Reaction score
126,553
Hakuna mwanamke ambaye hajawahi kuvaa khanga, vilevile hakuna mwanaume ambaye hajawahi kufunikwa na khanga (utotoni si ulibebwa )....Yafuatayo ni maajabu ya khanga

1/Historia
Asili ya vazi hili ni pwani ya Afrika Mashariki kama sehemu za Mombasa nchini Kenya na visiwani Zanziba. Ndio walikuwa watu wa kwanza kulivaa vazi hili na kuliheshimu.Haijajulikana ilikuwa ni miaka gani. Kwahiyo historia inaonyesha vazi la khanga limeasisiwa na watu wa pwani ya Afrika Mashariki

2/Fahari ya Mwafrika
Khanga ni fahari kwa wanawake wa kiafrika , Ni vazi ambalo limetumiwa miaka kwa miaka, kizazi kwa kizazi.....ni utambulisho wa waafrika na halichuji !!

3/Linapendwa na rika zote
Khanga ndio vazi linalopendwa na wanawake wa aina zote, vijana kwa wazee, mjini kwa vijijini ....ni mwendo wa kutupia khanga !!

4/Matumizi kibao
Khanga ni vazi lenye matumizi mengi pengine kuliko yote, linatumika kubebea watoto, kufungia ngata,kama kamba.taulo n.k

5/Khanga moko ni shida
Wanawake wakitupia khanga moko mwanaume lazima utoe jicho , khanga moko uswahilini ni balaa hadi kwenye vigodoro....mwanamke khanga!!!

6/Vazi linalosema
Khanga huwakilisha hisia za mvaaji kupitia maneno yaliyoandikwa, kuna vijembe, busara,matusi, hekima n.k


The Bitoz
 
Afadhali ile iloandikwa tulia mkwaju waja kuliko hiyo ya wake wanne
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mbavu zangu zinauma
 
Panua paja, mkwaju waja..

Salama wa Mkasi anaupenda sana huo msemo! Teh teh! Heshima yako mkuu Jimena
Hahahahahaha asante mkuu
Shukrani kwa kunisahihisha pia

Ni moja kati ya khanga yenye maneno maridhawa kabisaaaa[emoji85] [emoji85]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…