Maajabu ya kuku(wa kienyeji)

Full 8

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
313
Reaction score
271
Igweeee..

Ni matumaini yangu mu-wazima wa afya.


Naamini wafugaji wakuku mnatambua uwezo mkubwa wa kuku katika kutambua hatari iliyo mbele yake; kama vile mwewe, kipanga, mbwa, paka, nyoka na kadharika.
Mara ikitokea hatari yoyote kuku hutoa ishara ya sauti kwa kuku wengine na mara moja huchukua hatua ya kukimbilia mahali salama. Ishara hizi huwa tofauti tofauti kulinganga na hatari yenyewe.


Uwepo wa mwewe/Kipanga.
Endapo kipanga/mwewe akiwa karibu utasikia kuku wakitoa sauti flani hivi ( kruuuu kruuuu....) ukifatilia utamwona anapita maeneo hayo.
Kinachonishangaza ni pale anapotoa sauti ila ukitazama angani unaweza usimwone mwewe/ kipanga ila sekunde kadhaa baadae anaonekana akitokea upande mwingine wa nyumba.

Swali.
1. Kuku wanatumia mbinu gani kutambua hatari zinazowakabili ukiachana na macho, kwani wanaweza kutoa ishara hata kabla hatari kuonekana kwani kuna wakati kuku wako ndani lakini wakahisi hatari iliyo nje ya nyumba.
2.Ishara nyingi huzitoa Jogoo, je jogoo ana uwezo mkubwa wa kutambua hatari zaidi ya mitetea?


Nawasilisha.
 
jogoo anasignal inyosoma zaidi ya 4G
 
Inasemekana ule msmeno juu ya kichwa cha jogoo ni antena yenye uwezo mkubwa balaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni maajabu ya uumbaji wa Mungu.
Hata wewe ukipita sehemu yenye hatari kama chui au fisi, nywele za kichwa zinasimama alafu kuna shock inapita mwilini lazima uongeze spidi hapo hata hujamwona huyo mnyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…