Mzalendo_Mkweli
JF-Expert Member
- Jan 30, 2012
- 2,025
- 1,270
Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Caf , CS Constantine wa Algeria itakuwa timu ya kwanza kwa robo fainali ikiwa wataepuka kushindwa Ijumaa nyumbani wakati wakicheza na Club Africain ya Tunisia.
Baada ya kuishinda Club Afrika mjini Tunis kupitia goli la dakika za lala salama la Abdenour Belkheir, klabu iliyoanzishwa mwaka 1898 ina sababu za matumaini katika mchezo utaochezwa ijumaa ya leo.Lakini kocha wa CS Constantine aliyezaliwa Ufaransa Denis Lavagne anaiangali kwa jicho la tahadhari Club Africain ya Tunisia iliyo katika nafasi ya tatu katika kundi ambayo inapaswa kushinda mechi ya leo kurudi kwenye harakati za kumaliza katika nafasi mbili za juu za kundi lao.
"Tunaweza kuhitaji pointi moja tu kufikia robo fainali lakini hatutaidharau Club Africain kwa sababu ni mechi ya kufa au kupona kwao," aliviambia vyombo vya habari vya Algeria.
Kama Constantine angalau itapata sare mbele Club Africain ya Tunisia , mabingwa wa mara tano TP Mazembe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia watafudhu kutoka Kundi la C kama tu wataepuka kushindwa Ismaily yaa Misri.
Kwa ujumla wake hali katika makundi yote manne yapo kama ifuatavyo
GROUP A
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa wa 2016 na 2017,zitaendelea robo fainali ikiwa watashinda mechi zao wiki hii.
Viongozi wa Sundowns wanawakaribisha Lobi Stars ya Nigeria huko Pretoria na wanatarajia kiwango kizuri cha mchezaji aliyesainiwa hivi karibuni toka Argentina Emiliano Tade kitawezesha kusonga mbele.
Wydad ina kazi ngumu zaidi watakapo pambambana na mabingwa wa zamani ASEC Mimosas wa Ivory Coast, ambao wanapaswa kushinda hii mechi ili kuendelea kuweka hai matumaini yao ya kusonga mbele katika robo fainali na kwa vile pia wanataka kulipiza kisasi cha kufungwa 5-2 huko Morocco.
GROUP B
Mapingwa wa sasa Esperance wa Tunisia wanaweza kupata nafasi ya robo fainali kwa kuishinda Horoya AC ya Guinea ambapo katika mechi ya kwanza ya kundi hilo Esperance waliishinda Horoya AC ya Guinea
Vurugu ya katika michuano michuano ya Ligi ya Mabingwa ya msimu uliopita imesababisha mechi mbili za Esperance kucheza nyuma ya milango imefungwa (bila mashabiki), ambazo Esperance ilizishinda zote kwa mabao mawili.
Orlando Pirates ya Afrika Kusini wanatarajiwa kushinda FC Platinum ya Zimbabwe ambao tayari wameshaondolewa katika mashindano hayo ingawa bado wabebakiwa na mechi ya mwisho dhidi Horoya AC ya Guinea
GROUP C
Constantine, iliyo kundi lenye mabingwa watatu wa zamani, wana rekodi bora ya vilabu vyote 16 katika makundi yote manne kwa kupata pointi 10 kutokana na mechi nne walizocheza. Cha kushangaza, magoli 12 yaliyofungwa na hao Waligeria katika mechi za kikundi yametokana na wachezaji 11 huku beki wa kati Nasreddine Zaalani akiwa amefunga mara mbili. Timu yenye wachezaji kutoka mataifa mbalimbali ya TP Mazembe yenyewe imekuwa na matokeo yasiyotabirika sana kwani waliishinda Club Africain 8-0 nyumbani na kufungwa 3-0 na Constantine.
GROUP D
Ni pointi tatu tu zilizopo kati viongozi hili kundi mabingwa mara nane Al Ahly ya Misri na timu iliyopo ya chini ya Vita Club ya DR Congo ambayo inashika nafasi ambayo haikutarajiwa katika hili kundi.
Ahly imepoteza mechi mbili kati ya tatu ilizocheza ugenini katika mechi za Ligi ya Mabingwa msimu huu hivyo hawawezi kuhamasika na kuwa ujasiri sana kabla ya kupambana na Vita Club huko Kinshasa kunakoogopesha timu nyingi zinazoenda huko..
Simba SC ya Tanzania ina rekodi ya kushangaza katika kundi hili kwani mara mbili imefungwa 5-0 katika mechi zao za ugenini. Ingawa inaonekana Simba SC wanaweza kufungwa magoli machache zaidi dhidi ya JS Saoura wa Algeria, hata hivyo kufungwa ni jambo linaloonekana ni dhahiri kwao
Source : Caf Champs League surprise side on course for quarters