Maajabu ya maabara ya hospitali zetu!!!

Maajabu ya maabara ya hospitali zetu!!!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,652
Hiki kituko nimekishuhudia leo baada ya ndugu yangu kwenda kwenye hospitali tatu tofauti na kupata majibu ya vipimo vya malaria tofauti kwa 'case' moja ile ile.

Kwamba alienda kwenye maabara A ya health centre moja, akaambiwa ana 4 MPS (yaani ana vijidudu vya malaria 4), lakini akaamua kwenda kwenye maabara nyingine B aliyowahi kupima mwanzoni, majibu aliyoyapata hapo akaambiwa hana malaria yaani alionekana ana O MPS. Akaona aende kwenye maabara nyingine C, huko nako majibu yakawa kwamba hana malaria, yaani O MPS.

Binafsi nimebaki hoi baada ya kuambiwa haya maneno. Hivi kwa mtindo huu tutabaki salama kweli wandugu? Hebu jipe muda kuwaza hii 'maneno'.
 
ulikuwa hujui kuwa maabara zetu zipo kisanii wenyewe wakijisikia kuchoka tu haaooo wanakwea pipa kufanyiwa checking ya afya india
 
Back
Top Bottom