Maajabu ya orodha ya tisa kwenye maisha ya mwanadamu

Maajabu ya orodha ya tisa kwenye maisha ya mwanadamu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
MAAJABU YA TEBO YA TISA KWENYE MAISHA YA MWANADAMU


9×1=9 miez ya kuishi tumboni

9×2=18 umri wa kutambulika mtu mzima kwa baadhi ya nchi

9×3=27 miaka ya ukomavu na binadam kijana anaweza anza kunitegemea kila kitu makazi,malazi na mengneyo

9×4=36 miaka ya kuweza muda kulea( kuanzisha au kuwa na familia yake)kiongozi kabisa

9×5=45 hii miaka hekima huendelea kukomaa na ujuzi wa mambo kwa upana huongezeka ni miaka sahihi sana kuweza kuwa kiongozi wa familia, kampuni,taasisi,vyama n.k


9×6=54 miaka ya busara hekima,na tamaa nyingi za mwili huisha kwa walio wengi, pamoja na nguvu za mwili kupungua lkn akili maarifa huwa kubwa ndio kipindi sahihi pia kuweza kuwa mkurugenzi wa taasisi yoyote kubwa na hata kuongoza nchi, maana mihemko na sifa kupungua

9×7=63 miaka ya toba na kujiandaa kuwa mzee mwema na mwisho mzuri kwa kuanza pia kujisogeza sana kwa Mungu na pia ndio umri mzuri pia kuongoza watu maana akili na moyo huwa hazina tamaa kama kijana wa miaka chini ya miaka 30 mwenye ndoto nyiingi na nadharia kibao negative



yanayotokea kwa vijana hawa ni sababu ya kuwahisha kuwapa nafasi kabla ya umri mazingira na tabia za binadamu
 
😂Huo u'ajabu hapo uko wapi ?

ingalikua it's constant to each one of us, hapo ungekua sahihi sana.
Its only the first one( 1 x 9 =9 ) that hold the rest ni blah blah.
 
September ndio mwezi pekee ambao unaendana na number 9.Neno september lina herufi 9.Miezi mingine haiko hivyo



9 Ni namba ya ajabu sana chukua namba zozote tatu mamia zisizo na zero zinazogawanyika kwa 9 .Mfano 567

Hii namba waweza igeuza utakavyo utashangaa bado inagawanyika kwa 9

mfano 567 waweza igeuza mpangilio ikawa 576, 657, 675, 756, na 765 utakuta zote zinagawika kwa 9





uhuru wa Tanzania tuliopata tarehe 9 december1961

SEPTEMBER 11 word trade centre MAREKANI ILIPIGWA NA MAGAIDI

Kundi moja la kigaidi huitwa black september
 
Sasa hivi mama amefanya tuache siasa za kizamani afadhari mama achukue 2025 ..kuliko wababa tupumue
 
Haha haha hahahah
Awali nikiwa mdogo, nikiwa na kama miaka 13 hivi, nilikuwa napenda sana kusoma vitabu vya Science Fiction vya Dr. Isaac Asimov.

Siku moja nikawa nasoma habari moja kaandika, akidai anaweza kuonesha uhusiano wa kinamba kati ya Biblia na Solar System.

Akaanza kutaja habari zake pale, anakwambia sijui Biblia ina vitabu vingapi, ukichukua namba ya vitabu ukaifanyaje, unapata ratio ya umbali wa sayari katika slar system, ukichukua namba fulani kwenye biblia iankuonesha hiki kwenye Solar System.

Nikaona kataja namba nyingi sana na kaziwekea uhusiano mzuri sana kati ya biblia na Solar System.

Nikasema hili jambo linawezekana kweli?

Nikasema huyu Dr. Asimov anaheshimika sana, na namba alizotaja ni za kweli, inawezekana kabisa alichoandika ni kweli.

Nilivyoanza kumuamini tu, hapo hapo Dr. Asimov naye akawa kama kashajua kufikia hapa atakuwa kashanichota akili.

Akaiumbua habari nzima kwa kusema kaitunga tu mwenyewe, si ya kweli.Kwamba ukimpa mtu mwenye akili ya kuunganisha vitu dataset yenye data ya kutosha, kama biblia an Solar system, anaweza kuonesha uhusiano wa kihesabu kwa sababu ya ukubwa wa dataset tu, akakufanya uamini kwamba kuna siri za Solar System zimekuwa coded kwenye biblia.
 
Ni table nyepesi zaidi kuikariri wakati wa kujfunza.

Ila cha ajabu zaidi, 9x4=?
Jibu lake likiwa ndiyo umri wako. Sahau kuhusu mikopo inayotolewa kwa vijana kupitia mfuko wa Maendeleo ya Jamii.Sijui kwanini waliamua hivyo.

9x5= 45. Ukifika umri huu hujapata connection, matumaini ya kutoboa yanaanza kupungua.

9x6= 54. Umri huu kama hautapunguza michepuko, jiandae kutofaidi pension yako.
 
Back
Top Bottom